The House of Favourite Newspapers

Julitha Kabete Kukanyaga Miss World ni Mungu tu!

Mrembo ambaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindo ya Miss World 2017, Julitha Kabete.

 

MREMBO ambaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindo ya Miss World 2017, Julitha Kabete amesema kuwa mpaka kuweza kupata nafasi ya kwenda kuiwakilisha nchi yake sio kazi ndogo kama watu wanavyodhani kwani ameenda kuonesha ulimwengu kuwa hata taifa lake linaweza, haliko nyuma kitu ambacho kilimfanya asilale kwa ajili ya kuhakikisha anarudi na kitu ambacho kitaacha alama ya nchi yetu.

 

Mrembo huyo amefanya mahojiano na Mikito Nusunusu na kuongea mengi kama ifuatavyo hapa chini:

Mikito Nusunusu: Ni kitu gani kilikufanya uamue kwenda kushiriki Miss World nani alikusuma kufanya hivyo?

Julitha: Miss World ilikuwa ndoto yangu tangu niko mdogo sana. Pia nilivyozidi kukua niliona kua platform ya Miss World itanisaidia kujenga brand yangu na future. Kilichonisukuma sana, ni jinsi nilivyopanga mipango yangu ya miaka mitano mpaka 10 na nilijiona ninaweza kufanya kati ya miaka 19-20 na nilifanikiwa kushiriki miaka hiyo wakati naendelea na chuo. Sana nilijisukuma mwenyewe kabla ya mtu yeyote.

Mikito Nusunusu: Ni kitu gani kilikufanya usiweze kurudi na taji hilo ukiangalia na wewe una vigezo na vipi ilipofika huko kwenye mashindano?

 

Julitha: Taji la Miss World tulikuwa tukiwania washiriki 120. Kuna vipengele vingi vya kushindana lakini kwa nilivyona mimi, sapoti ya juu sio tu kutoka kwa wananchi pia serikali sapoti yao inahitajika. Mimi sikuenda kama Julitha Kabete, nilienda kama Tanzania. Na hapo nilibeba kitu kikubwa sana. Sio kitu kirahisi kama watu wanavyoona au kudhani. Nilijitahidi kwa uwezo wangu na kuingia Top 20 Beauty With Purpose. Wengi hata recognition hawapati. Namshukuru Mungu kwa hicho pia unaweza usibebe taji lakini sababu ya sifa unaondoka na vitu vingine vikubwa, makampuni mengi yanataka kufanya kazi na wewe na vitu vingi ambavyo vinaweza kukufikisha kimataifa.

Mikito Nusunusu: Ni kitu gani umeweza kujifunza huko?

Julitha: Ushirikiano na upendo. Nimekutana na wasichana ambao wana upendo na ushirikiano sana kitu ambacho napenda sana. Kwa hiyo nilifurahi kuwa kwenye mazingira kama yale. Pia nimejifunza kuwa, sapoti ni muhimu sio tu kwa wananchi bali serikali. Ila kupata sapoti kama hiyo lazima mashindano yawe mwanzo wa mwaka ili nchi ipate kumjua mrembo wao vizuri.

 

Mikito Nusunusu: Nani alikuwezesha kwenda huko kuanzia mavazi na gharama zote kwa kuwa najua hilo ni moja ya tatizo kubwa la Kamati ya Miss Tanzania kumuandalia vitu mrembo anayeenda kushiriki mashindano hayo?

Julitha :Nilipata sapoti kwa Kamati ya Miss Tanzania, Basata, familia yangu na makampuni mbalimbali kama Turkish Airlines. Kuhusu designers, nilitafuta mwenyewe, nilikuwa na mwezi mmoja tu wa kujiandaa. Huwa napenda niwe tofauti, sipendi kufananishwa hasa kwenye mavazi. Napenda kufuatilia designers wa kimataifa pia napenda kusapoti wa Tanzania as well lakini sipendi kurudia designers sana. Nilitafuta designers unique na wanaoendana na mapendekezo yangu.

Alipokuwa naongea na wanahabari.

Niligharamia baadhi ya designers kama nguo za usiku nilivaa sana za Dona Matoshi (International Designer) na wa Tanzania (Kiki).

Mikito Nusunusu: Ulishawahi kushiriki mashindano mengine makubwa zaidi ya Miss World?

Julitha: Ndio, nilishiriki Miss Afrika 2016, lilifanyika Calabar, Nigeria. Lilikiwa shindano la kwanza kuzinduliwa huko Nigeria na nilichaguliwa chini ya Millen Magese Organization. Niliingia Top 5 Finalist Representing East Africa.

 

Nusunusu: Nini matarajio yako ya baadaye na pia kuhusu ushirikiano kutoka kwenye familia yako wanapendezwa na kazi unayoifanya?

Julitha: Kwanza kuwasaidia vijana kupata ajira, pili nina ndoto ya kufungua na kukuza brand ambayo itakuwa na kiwanda cha kutengeneza products za urembo kama high-end perfume, skincare products na vipodozi. Vinginevyo mtaviona huko mbele ila ndoto yangu ni kukuza brand kubwa ya urembo na kuajiri vijana kujifunza na kuwa part ya brand yangu.

 

Kuhusu sapoti kutoka kwa familia ipo tangu nimeanza Miss Tanzania ila ilikuwa vigumu sababu nipo chuo huku nafanya mashindano kwa hiyo ilichukuwa muda kunisapoti lakini nimeipata walivyoona jitihada zangu.

Mikito Nusunusu: Una mpenzi? Kama ndio, anachuliaje unachofanya?

Julitha : Sina mpenzi, bado nafanya vitu vyangu vya maendeleo.

Mikito Nusunusu: Una matarajio ya kupata mtoto au urembo ndio utakuwa umechukua sehemu kubwa ya maisha yako?

Julitha : Of course Mungu akipenda, lakini sio muda wowote wa sasa, labda miaka 6-7 inayokuja Mungu akiendelea kunipa baraka za kuishi.

Mikito Nusunusu: Mashindano ya Miss Tanzania ni kama yanaelekea shimoni unafikiri nini kifanyike?

Julitha: Sidhani kuwa yapo shimoni lakini yapo kwenye wakati wa kuhitaji marekebisho mengi. Kama ni msaada waombe na kuweza kutoa Miss Tanzania event kama zamani ili kurudisha uaminifu kutoka kwa watu.

Mikito Nusunusu: Ni kwa nini wewe ndio uliteuliwa kwenda kushirikia Miss World na wakati wewe sio mshindi wa Miss Tanzania?

Julitha: Nilikuwa tano bora Miss Tanzania 2016. Na 2017 ilitakiwa mtu asiende sababu ya vitu vingi Miss Tanzania kamati inajua kiundani sasa kuokoa brand yao na muda waliokuwa nao kuchagua mrembo aende Miss World, ulikuwa mdogo, kwa hiyo waliruhusiwa na Miss World Organization kumchukua yeyote wa Miss Tanzania Top 5 wa mwaka 2016 kwenda Miss World 2017. Kutoka na sifa na vigezo walinichagua, pia uwezo wa kujiandaa mwezi mmoja wengi waliona mgumu kwangu nilivyoulizwa sikuona ugumu sana.

Niliona ni opportunity yangu na pia nilitaka kuonyesha vijana jinsi ya kushirikina na kampuni nyingi tu sio kutegemea kusaidiwa bali uwe na nguvu ya kutafuta. Kwa hiyo mimi kukubali kuwakilisha nilijipa mtihani mkubwa pia.

Mikito Nusunusu: Ni warembo gani hapa nyumbani wanakuvutia na unafuata nyayo zao?

Julitha: Ninavutiwa na hawa wachache kwa jinsi wanavyojiweka; Faraja Nyalandu, Jacqueline Mengi, Nancy Sumari, Brigitte Alfred, Flaviana Matata, Jokate Mwegelo na Millen Magese.

Mikito Nusunusu: Nakushukuru sana Julitha.

Julitha : Asante sana!

STORI: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi

 

Comments are closed.