The House of Favourite Newspapers

Jumba La Dhahabu: Msimu Wa Pili Waja Na Msisimko Mpya! – Video

MR CHUZI

Muigizaji na muongozaji wa filamu nchini, Tuesday Kihangala maarufu kwa jina la Mr. Chuzi, amewataka Watanzania na wapenzi wa filamu kukaa mkao wa kula, kwani hivi karibuni ataachia filamu mpya inayosubiriwa kwa hamu, “Jumba la Dhahabu: Season Two.”

Mr. Chuzi ameeleza kuwa msimu huu wa pili utakuwa wa kipekee na wa kusisimua zaidi kuliko wa kwanza, huku akisisitiza kuwa filamu hiyo itakuwa na msisimko mkubwa na mafundisho yenye maadili kwa jamii.

Miongoni mwa washiriki wanaotarajiwa kung’ara katika msimu huu ni wasanii maarufu, Jini Kabula na Mzee Chilo, ambao wamejizolea umaarufu kwa uigizaji wao bora na wenye mvuto.

Mashabiki wa filamu hii wanashauriwa kufuatilia kwa karibu ili wasikose kuona ubunifu mpya na burudani ya hali ya juu ambayo Mr. Chuzi ameandaa kwa ajili yao.