testiingg
The House of Favourite Newspapers

Jumuiya Ya Wazazi CCM, Dar Ilivyoazimisha Miaka 46 Ya CCM

Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Dar, atia neno

0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Temeke, Hamis Slim akipanda mti kwenye shule ya Sekondari ya Vituka katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa CCM.

Dar es Salaam 29 Januari 2023: Katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) jana Jumamosi Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam imefanya maadhimisho hayo kwa kufanya usafi, kupanda miti na kukagua miradi ya madarasa mapya yanayoendelea kujengwa katika wilaya ya Temeke.

Jumuiya hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Khadija Ally Said na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Temeke, Hamis Slim, ilimpokea Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Bara, ndugu Daniel Savi aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, ndugu Daniel George Savi (kulia) akitoa maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa Lumo Sekondari, Frida Kyando alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa mapya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar, Khadija Ally Said akisikiliza kiumakini.

Maadhimisho hayo yalianza yalianza na zoezi la usafi na kupanda miti katika Shule ya Sekondari ya Vituka na kisha kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo kusikiliza changamoto zao.

Baada ya hapo msafara huo ulielekea Sekondari ya Lumo ambayo inaendelea na ujenzi wa madarasa mapya baada ya kupewa fungu la zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya kuendeleza madarasa.

Ukaguzi ukiendelea katika Sekondari ya Lumo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Dar na mgeni rasmi wakiwa na wajumbe wa kamati tendaji walioneshwa mradi huo unavyoendelea na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Frida Kyando.

Baada ya kuukagua mradi huo walienda kuikagua Shule ya Sekondari ya Kilimahewa ambayo wazazi walijichangisha na kuifanyia ukarabati shule hiyo kwa kuipaka rangi na kuwa na muonekano wa kuvutia na kuifanyia ukarabati sehemu mbalimbali ikiwemo madawati.

Ukaguzi wa ujenzi wa madarasa mapya ukiendelea.

Baada ya hapo wajumbe hao walielekea Ukumbi wa Chuo cha Bandari uliopo Tandika na kuzungumza na wanachama waliofurika kwenye maadhimisho hayo.

Kabla ya kumkaribisha mgeni kuzungumza mbele ya wajumbe wa kamati tendaji na wanachama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar (Khadija) aliwaeleza wanachama waliokusanyika ukumbini hapo jinsi alivyofurahisha miradi waliyoitembelea kwa pesa zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu na kuendelea kusema;

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally Said akizungumza na wajumbe wa kamati tendaji na wanachama wa CCM (hawapo pichani) kwenye Ukumbi wa Chuo cha Bandari Tandika, Dar.

“Sisi kama jumuiya ya wazazi nna imani kubwa kuwa miaka yetu mitano tuliyopewa kwa umoja wetu tutafanya kazi kubwa na kukiheshimisha chama chetu ili kiwe mfano wa kuigwa.

“Jumuiya ya Wazazi Temeke nawashukuru sana kwani nimegundua kuwa tunaimba wimbo mmoja, maana vinginevyo kama kiongozi wa mkoa una dira nyingine na viongozi wako wa wilaya nao wana dira yao tofauti hamuwezi kufika popote katika suala la maendeleo.

Wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani nao walijitokeza na kupewa kadi na kula kiapo.

“Kwa mwendo huu mnaouonesha Temeke nna imani tutaiimarisha jumuiya yetu na chama kwa ujumla na kuhakikisha tunazidisha imani kwa wananchi na kupata ushindi mkubwa katika nafasi zote katika uchaguzi mkuu ujao na kumrejesha Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu anayeendelea kuing’arisha nchi yetu na kuendeleza amani na upendo.

“Mama Samia oyeee.” Alimaliza kusema Mwenyekiti Khadija na kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Jumiya ya Wazazi CCM Bara, Daniel George Savi.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo mgeni rasmi aliwataka wanachama wa CCM kuwa mfano bora kwa jamii ili kujenga heshima na kuzidisha imani ya wananchi katika chama.

Akiendelea kuzungumza aliwageukia viongozi wa kamati tendaji na kuwaambia;

“Viongozi tuliopewa nafasi tuzitendee haki dhamana tulizopewa kwa kutimiza wajibu wa kuwatumikia wananchi.

“Daniel aliwasisitiza viongozi hao kuwa mfano bora na kukipa heshima chama ili hata katika uchaguzi mkuu ujao watu wanaopenda kukosoa bila kusifia hata inapobidi wakose la kusema na kukichagua chama cha Mapinduzi katika nafasi zote”. Alisema.

HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS GPL

Leave A Reply