Jumuiya ya Wazazi CCM Kata Azimio Dar, Yatoa Msaada Zahanati Tambukareli
Dar es Salaam, 7 Januari 2023: Jumuiya ya wazazi Kata ya Azimio Temeke, Dar leo imetoa msaada wa vifaa tiba kwenye Zahanati ya Tambuka reli iliyopo kwenye kata hiyo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Katibu wa Wazazi Kata ya Azamio ambaye ni Kaimu Katibu wa jumuiya hiyo Wilaya ya Temeke, Tukae Kondo amesema kabla ya kutoa msaada huo walitembelea kwenye Zahanati hiyo na kubaini changamoto ya vitanda vya kujifungulia na mengineyo.

Tukae amesema baada ya kubaini hilo ndipo wameanza na kutatua changamoto hiyo pamoja na vifaa tiba kadhaa walivyotoa kwenye hafla hiyo.

Tukae amesema huo siyo mwisho wao wa kuisaidia Zahanati hiyo na kusisitiza kuwa huo ni mwanzo tu na wataendelea kuisaidia zahanati hiyo na maeneo mengine kwenye kata hiyo.

Msaada huo ni pamoja na kitanda cha kujifungulia, mashuka, dawa za kufanyia usafi na vitu vingine. Wanachama hao kabla ya kutoa msaada huo walianza na zoezi la kufanya usafi maeneo ya hospitali hiyo na kumalizia na zoezi hilo. HABARI/ PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL