The House of Favourite Newspapers

Juve yashinda, Ronaldo akosa penalti

TIMU ya Juventus juzi iliendelea kujikita kileleni kwenye Ligi Kuu ya Italia baada ya kufanikiwa kuichapa Chievo mabao 3-0 kwenye mchezo wa Serie A.

Juventus ambao wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu kwa sasa wapo kileleni kwa tofauti ya pointi tisa dhidi ya Napoli iliyopo nafasi ya pili huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 20.

 

Cristiano Ronaldo alikosa penalti kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Dimba la Allianz, ambapo mabao ya Juventus yalifungwa na Douglas Costa, Daniele Rugani na Emre Can. Kipa wa Chievo, Stefano Sorrentino, amekuwa wa kwanza kuokoa mkwaju wa penalti wa Ronaldo kuanzia alipojiunga na Juventus mwanzoni mwa msimu huu.

Comments are closed.