Juventus na Monaco Wazifuata Atletico na Real Madrid Nusu Fainali UEFA

Wachezaji wa Barcelona wakiongea na refa huku mchezaji wa Juventus, Higuain akiwaangalia.

Alianza Kylian Mbappe kucheka na nyavu za Dortmund akishuhudiwa kufunga mara 4 mfululizo katika michezo yake minne ya mwanzo katika hatua ya mtoano ha Chamipons League.

Baadae Radamel Falcao “El Tigre” alifunga lingine na kuifanya Monaco kumaliza mchezo huo na ushindi wa bao 2 kwa 1 huku lile la Borussia Dortmund likiwekwa kimiani na Marco Reus.

Lakini kule Nou Camp katika mchezo uliokuwa ukiangaliwa na wengi kati ya Barcelona na Juventus ilishuhhdiwa Barcelona wakiondolewa katika michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana nyumbani kwao.

Katika mchezo wa kwanza klabu ya Barcelona ilikufa bao 3 kule Italia na matokeo ya suluhu yamewafanya kuondolewa katika michuano hiyo kwa aggregate ya bao 3 kwa 0.

Kipa wa Barcelona, Marc-Andre akiwa hoi baada ya kutolewa na Juventus.

Matokeo hayo yanazifanya Juventus na Monaco kufudhu katika hatua ya nusu fainali wakiifuata Real Madrid na Atletico Madrid ambao wao walitangulia katika hatua hiyo ya nusu fainali ya michezo hiyo.

Nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo itachezwa tarehe 2 na 3 ya mwezi wa tano kabla ya marudiano yatakayopigwa tarehe 9 na 10 mwezi ujao, na watakaofudhu watakutana uwanja wa taifa wa Wales tarehe 21 mwezi ujao kwa ajili ya fainali.

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment