Juventus Yajitupa kwa De Gea

KLABU ya Juventus ambayo imekuwa ikifanya usajili wa kufuru kwa miezi ya hivi karibuni, inajiandaa kumsajili kipa wa Manchester United, David de Gea.

 

De Gea amekuwa akiwindwa na timu kadhaa kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na ubora wake langoni. Timu za Real Madrid, PSG na Barcelona zimekuwa zikitajwa mara kwa mara kuwa zinataka saini ya kipa huyo raia wa Hispania.

 

Hata hivyo, sasa inaonekana kuwa Juventus itakuwa na nafasi kubwa sana ya kumtwaa kwa kuwa kipa huyo bado hajasaini mkataba mpya na timu hiyo na mkataba wake unaelekea ukingoni. Kama kipa huyo hatasaini mkataba mpya hadi Januari basi kwenye usajili mkubwa ataondoka bure.

 

De Gea anaaminika kuwa anataka mshahara wa zaidi ya pauni 350,000 (Sh mil 986) kwa wiki ili abaki kwenye kikosi hicho, lakini bado hawajakubaliana na Man United.


Loading...

Toa comment