The House of Favourite Newspapers

Jux Afunga ndoa na mpenzi wake, Priscyla, raia wa Nigeria – Picha

JUMA Jux; ni msanii maarufu wa RnB kutoka Tanzania, amefunga ndoa na mpenzi wake, Priscyla, raia wa Nigeria, katika hafla ya kifahari iliyofanyika hivi karibuni.

Sherehe ya kipekee ya ndoa hiyo imefanyika jana Februari 7, 2025 ilihudhuriwa na familia, marafiki wa karibu, pamoja na baadhi ya mastaa wa Bongo Fleva, wakiwemo Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ambaye ni CEO wa Lebo ya WCB, na wengine wengi.