The House of Favourite Newspapers

Jux Aweka Maneno Sawa Kuhusu Kuhusishwa Kimapenzi na Paula

0
Mrembo Paula, Mtoto wa Kajala Masanja

JUMA Jux; ni staa kabisa wa muziki wa RnB kutoka nchini Tanzania ambaye ameweka maneno sawa kuhusu kile kinachodhaniwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi baina yake na mrembo Paula Kajala ambaye ni mtoto wa muigizaji Kajala Masanja; pisi ya Konde Boy.

Jux anasema kuwa, kuwa uhusiano wake na binti huyo wa kambo wa msanii Harmonize ni wa kibiashara tu na wala hawajawahi kuvuka mipaka na kuzama kwenye penzi hata siku moja.

Staa huyo anaitetea video ambayo ilidaiwa kuwa Paula alionekana akiingia nyumbani ambapo anasema kuwa hata hajawahi kufika katika makazi yake.
Jux anasisitiza kwa kumtaja Paula kama dada yake mdogo na wala hawezi kuingiwa na suala la kumuomba kuwa wapenzi.

Jamaa huyo anahitimisha kwa kusema kuwa, kwa yupo kwenye uhusiano mwingine ambao unampa amani ya akili kupita maelezo.

Mkali wa RnB Nchini Tanzania, Juma Jux

“Ninachoweza kusema ni kama dada yangu mdogo. Hajawahi kuja nyumbani kwangu. Sijawahi kuona hiyo clip. Ndiyo, kwenye clipu inaonekana kama nyumba yangu.

Sikumbuki ni muda gani nilimuona. Ukweli ni kwamba, yeye ni msichana mdogo ambaye namuona akifanya mambo yake. Hatuko kwenye uhusiano kwa sababu niko kwenye uhusiano wangu mwenyewe,” anasema Jux; mkali wa Ngoma ya Kiss aliyomshirikisha Marioo.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply