Jux, Lulu Diva Mambo Hadharani!

MAMBO ni moto! Hivyo ndivyo wanavyosema wananzengo kufuatia tetesi za kuchipuka kwa penzi jipya na matata mjini likiwahusisha mastaa wawili wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’ na Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

Tetesi zilizosambaa wikiendi iliyopita zilieleza kuwa, wawili hao kwa sasa ni kitu na boksi baada ya kuwa wanaonekana mara kwa mara wakiwa pamoja kwenye gari, jambo ambalo limeibua minong’ono kila kona.

 

Jambo hilo limekumbusha tukio la siku za nyuma ambapo wawili hao walidaiwa kuondoka pamoja kwenye gari la Jux baada ya kushuti video maeneo ya Ubungo jijini Dar,

“Jux na Lulu Diva ndiyo kapo mpya mjini japokuwa wenyewe wanajitahidi kufichaficha, lakini ukweli utakuwa wazi muda si mrefu.

 

“Labda kama wanatoka na kumalizana kisirisiri, lakini ukweli ni kwamba mambo ni moto, acha watu watumie fursa,” kilidai chanzo kimoja ambacho ni mtu wa karibu na wawili hao.

Chanzo hicho kiliendelea kuweka wazi kuwa, kuna siku Jux na Lulu Diva walikuwa wakirekodi video maeneo ya Ubungo.

 

“Baada ya kurekodi, Lulu Diva alipanda kwenye gari la Jux na kuondoka pamoja kwenda kusikojulikana, sasa usiniulize huko walikwenda kufanya nini.”

Baada ya kusikia ubuyu huo wa mjini, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta Lulu Diva na kumsomea tuhuma hizo ambapo awali alishtuka kisha akawa anacheka mno.

 

Alipobanwa kusema anachokijua juu ya jamaa huyo, alisema hata kama ana uhuni kiasi gani, hawezi kutembea na Jux.

“Jamani hapo kwa Jux wamenisingizia. Siwezi kutembea na Jux kwa sababu nyingi tu.

 

“Ukweli ni kwamba, kwa hapo wamenibebesha tu, lakini mimi si wa hivyo. Ninamheshimu na tunaheshimiana, halafu watu hawajui tu, yule ni shemeji yangu,” alisema Lulu Diva bila kufafanua ni shemeji yake kwa nani.

 

Kwa upande wake Jux, simu yake iliita bila kupokelewa. Madai hayo kwa Jux yanakuja miezi kadhaa baada ya kutengana na Vanessa Mdee ‘V-Money’ na Nayika Thongom wakati Lulu Diva aliwahi kudaiwa kutoka na mastaa kama Jaquar wa Kenya, Rich Mavoko na TID ambao amekuwa akiwakana.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Toa comment