KIKOSI cha Kusini cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kimesema kitafanya msako katika misitu ya mikoa inayopakana na Msumbiji na ile iliyokaribu na nchi hiyo.
Kiongozi wa zoezi hilo amewataka wote waliopo katika misitu mikoani Lindi, Mtwara na Ruvuma kuondoka mara moja kupisha operesheni hiyo.
Amesema wataanzia Ruvuma na kisha kwenda Lindi kwa sababu kuna watu wanaofanya vitendo vya kihalifu ndani ya misitu hiyo.
Mwezi Mei mwaka huu Serikali ilisema itapeleka vikosi mpakani kuimarisha usalama kufuatia shambulio lililotokea eneo la Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji.
Shambulio hilo lilihusishwa na wapiganaji wa Dola la Kiislamu na ilidaiwa wapiganaji hao wameweka kambi Msumbiji, lakini Serikali ya nchi hiyo ilikanusha vikali madai hayo.