JWTZ Lapokea Ndege ya Kijeshi Kutoka Falme za Kiarabu (UAE)

Dar es salaam, 4 Februari 2025: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dk. Stergomena Lawrence Tax (Mb) leo amepokea ndege ya kijeshi kutoka Jeshi la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Falme za Kiarabu.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo Dk. ameshukuru na kusema ushirikiano huo uendelee kwa manufaa ya pande zote mbili.

Ameendelea kusema kutokana na kazi kubwa ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuona kwamba ushirikiano baina ya nchi hizi mbili unaimarishwa ambapo ndege hiyo itatumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo, kusafirisha viongozi mbalimbali wa kiraia na kiserikali, usafirishaji wa kijeshi na kudondosha askari wa miavuli.

“Mashirikiano haya yanayoendelea kati ya jeshi letu na jeshi la Umoja wa Falme za Kiarabu, serikali anayoiongoza rais wetu, Dk.Samia ni kudumisha mahusiano mazuri na nchi rafiki. Jeshi letu lipo tayari kutekeleza majukumu yetu ndani na nje ya nchi na kuhakikisha inakuwa salama”. Alimaliza kusema Waziri Tax. HABARI: NEEMA ADRIAN
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL