The House of Favourite Newspapers

JWTZ na Jeshi la India Wazindua Mazoezi ya Pamoja Washirikisha Nchi Rafiki 9

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax akizungumza na wanahabari baada ya uzinduzi wa mafunzo hayo.

Dar es Salaam, 13 Aprili 2025: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) leo amezindua zoezi la Africa India Key Maritime (AIKEYME) ambapo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ikishirikiana na Jeshi la Wanamaji kutoka India lengo likiwa ni kupambana na matishio ya uharamia, usafirishaji haramu wa binadamu, usafirishaji haramu wa silaha, madawa ya kulevya ikiwa ni ushirikiano wa nchi rafiki duniani.     

Askari wakiwa kwenye mazoezi ya baharini leo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mh.Tax (Mb) amesema zoezi hilo linalojulikana kama Africa India Key Maritime Engagement (AIKEYME) ambalo litashirikisha na Majeshi mengine ya nchi rafiki.

Askari wa majini wakiwa katika mazoezi ya majini leo.

Amesema Waziri huyo kuwa kwa sasa changamoto za uhalifu ulimwenguni zinafanana hivyo mafunzo haya ya pamoja yatakuwa na faida kubwa sana kwa nchi zilizoshiriki kwa kubadilisha uzoefu na kuzifanya nchi zetu kuwa salama.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jenerali John Jacob Mkunda akizungumza baada ya uzinduzi huo leo.  

 Zoezi hilo litawezesha vikundi shiriki kuongeza ujuzi na uelewa wa pamoja wa kukabiliana na changamoto za kiusalama hasa katika maeneo ya baharini.

Ukiachana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na India pia zimeshirikishwa nchini tisa zilizopakana na Bahari majeshi nazo yamekuja kushiriki ikiwemo Kenya, Afrika Kusini, Djibouti, Uganda, Tanzania, India, Msumbiji, Madagascar, Comoro, Shelisheli, Mauritius ambazo zimekuja na meli za vita na meli za utawala kwenye mafunzo hayo ya kupambana na matishio baharini.