JWTZ Waibuka Mshindi wa Jumla Mashindano ya Majeshi (BAMMATA)
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali, Salum Haji Othuman amemuwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali, Jacob John Mkunda kuwaongoza Wakuu wa Vyombo Vya Ulinzi na Usalama kufunga mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA).
Katika mashindano hayo yaliyofungwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Hamis Mwinjuma tarehe 15 Septemba 2024 Mkoani Morogoro JWTZ wameibuka mshindi wa jumla wa mashindano hayo.
Kutokana na ushindi huo Luteni Jenerali Salum Haji Othuman amepokea kombe hilo kwa niaba ya JWTZ.
Mashindano hayo ya wiki mbili yalizishirikisha timu kutoka JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Idara Maalum kutoka visiwani Zanzibar.