The House of Favourite Newspapers

K-LYNN ‘ACHOMOA’ KUTOA BURUDANI

MREMBO aliyewahi kutamba kwenye anga la Kizazi Kipya akitumia jina la K-Lynn, Jacqueline Ntuyabalilwe (sasa hivi Jacqueline Mengi) juzikati alichomolea ishu ya kutoa shoo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mshereheshaji wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Malkia wa Nguvu.

 

Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Posta, Dar ambapo baada ya mwanadada huyo kumpa tuzo mmoja wa wanawake aliyeshinda Tuzo ya Malkia wa Nguvu ndipo mshereheshaji, Mussa Hussein akamtaka atoe shoo kidogo kukumbushia enzi zake.

 

Jacqueline licha ya kuombwa kufanya hivyo na hata kubembelezwa aliendelea na msimamo wake na kusisitiza kuwa alifika jukwaani hapo kwa ajili ya kutoa tuzo na si kutumbuiza.

Comments are closed.