The House of Favourite Newspapers

K-Mziwanda Kutoka Kuwa Konda Hadi Uhamasishaji Simba

0

CHAMPIONI Jumatano, limekusogezea simulizi mzuri ya shabiki wa Simba, mwanadada ambaye kwa sasa amekuwa
maarufu mitandaoni kutokana na
maneno yake.

 

Ni yule aliyekuwa mhamasishaji Simba Day, lakini ni yule aliyezungumza akiwa na Mwijaku kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Mwijaku akitoa ahadi ya kutembea bila nguo kitaani.Dada huyo anajulikana kama K Mziwanda, mwandishi na mtangazaji ambaye kwa sasa yupo Mbengo TV.
Championi limepiga naye stori nakujua mengi kuhusu maisha yake.“Jina langu halisi ni Kessy au Kuruthum Hassan. Nimezaliwa mtoto wa kike pekee kwenye familia ya watoto wanne ya Mzee Hassan Omary Rhumba.“Tulizaliwa kwenye Kijiji cha Maramba jijini Tanga.

 

Mimi ni Mdigo wa Duga Maforoni mjukuu wa Mzee Beja wengi wananiita hivyo huko nyumbani.“Nina kaka zangu wanne, mimi ndiye wa mwisho kuzaliwa.

 

ALIVYOINGIA KWENYE MICHEZO
“Kuhusu michezo
nilianza kupenda toka nikiwa mdogo nikiwa nasoma shule ya msingi.“Wakati ule Halima
Mchuka (marehemu) akiwa
mtangazaji pekee wa mpira mwanamke redioni, kina Sued Mwinyi wakitangaza
mpira kwa uhodari
mkubwa Mbali na hayo pia Simba ndiyo ilifanya niongeze mahaba kweye soka, wakati ule Simba
ya moto, kina Ulimboka
Mwakingwe, Athuman Idd ‘Chuji’, wakaja kina Patrick Mafisango na wengine.

 

ALIWAHI KUCHEZA SOKA
“Huu mpira mbali ya
kuushabikia, nimeucheza sana, wakati nipo Shule ya Sekondari Agreement, pale
nilikuwa kiranja mkuu na
ikawa rahisi kuucheza toka kidato cha kwanza hadi cha tatu.

“Nilibahatika kuwa mchezaji muhimu na kiongozi kwenye timu ya shule ya wanawake, juhudi
zangu zikaonekana hadi
kuchaguliwa kuwa kwenye timu ya Mkoa wa Tanga kwenye mashindano ya Umiseta.

 

MAMA YAKE AMUWEKEA NGUMU
“Mama alikuwa hapendi
nicheze mpira kabisa na ikalazimika niache hayo mambo ya kucheza baada ya kufika kidato
cha
nne. Mtu pekee aliyekuwa ananisapoti alikuwa ni baba.

NI MTU WA DINI
“Nimelelewa kwenye
mazingira ya dini sana, kwetu ilikuwa ni bora usiende shule ila uende madrasa.

ALIKUWA NGUMI MKONONI
“Makuzi yangu yalikuwa
yamejawa ugomvi na ukorofi, ingawa napenda sana utani na ucheshi.

 

MARAFIKI ZAKE MASELA TU
“Sina marafiki wengi
wanawake, napenda kukaa sana na wanaume, kwa sababu wanawake mara nyingi ni
ngumu kujadili vitu vya msingi.

 

KWAO NI SIMBA TU
“Ukimtoa baba, wengine
wote pale nyumbani ni mashabiki wa Simba hadi mama, baba alijitahidi sana
kunivuta niwe shabiki wa Yanga
lakini ikashindikana.

 

KUMBE ILIBIDI AWE MJEDA
“Baada ya kumaliza shule,
baba alinifanyia mpango ili niende jeshini, kila kitu kilikuwa tayari ulikuwa
unasubiriwa muda tu ufike.


“Baadae ikabidi nije
Dar, lengo ilikuwa ni kuja kusomea udereva ili niende jeshini nikiwa na fani nyingine mbali na soka tu.

 

AIBUKIA KWENYE UTANGAZAJI WA RADIO
“Wakati nasomea udereva,
Times FM walikuwa wameanzisha shindano la kusaka mtangazaji wa redio. Nikaona
huenda ikawa fursa
kwangu.


“Kwa sababu
nilikuwa napenda sana kusikiliza redio na kuna wakati nikiwa peke yangu nikawa najifanya
mtangazaji au
kama kuna watu wamekaa sehemu nilipenda sana kuwahoji.

“Nikaenda kuchukua fomu ili niweze kushiriki na kujaribu bahati yangu. Nikakutana na watu zaidi ya 1000 ambao wanashiriki.

“Nifika hadi mchujo wa watu 30, kwa bahati mbaya nikatolewa kwenye mchujo wa kwanza wa fainali. Mashindano yalikuwa yanafanyika Dar Live Mbagala.

 

AGEUKIA UKONDA WA DALADALA
“Baada ya
kushindwa kwenye mashindano ikabidi nitafute kazi ya kufanya baada ya kukaa nyumbani kwa wiki tatu,
ikabidi niwe konda
wa daladala.


“Nikawa napakia
abiria kutoka Buguruni kwenda Chanika (Dar), wakati mwingine tunapiga ‘root’ ya
Buguruni hadi Makumbusho,
ilikuwa inanibidi niamke mapema na kuifuata gari Tabata Shule kila siku.

 

AHAMIA KWENYE SINGELI
“Nikaona ukonda wa
daladala pekee hautoshi, nikahamia na kwenye Muziki wa Singeli na nikawa
nimetoa wimbo wangu kwa
kwanza unaitwa Chawa.

 

SIMU YA E-FM YAMPA MCHONGO TIMES
“Ngoma yangu ya Chawa
ikawa kama tundu langu la kufanya kazi Times FM, nilipokea simu ya interview (mahojiano) juu ya wimbo wangu pale E-FM.


“Wakati najiandaa
kwenda kwenye interview, nikawa nimeweka ujumbe kwenye group (kundi) ambalo tulikuwemo washiriki wote wa shindano la kusaka vipaji.


“Mule kwenye group
kulikuwa na viongozi pia wakubwa wa Times, kumbe wao walikuwa na mpango
wa kunichukua kwani
walivutiwa sana na mimi licha ya kuwa sikufika mbali kwenye mashindano.

“Walivyoona ile taarifa ya kuwa nakwenda E-FM nafikiri walihisi naenda kufanya kazi, ikabidi wanipigie simu kuwa niende Times na wakawa wamenipa ajira moja kwa moja.


“Nilifanya kazi kwa miaka
minne, nikatangaza vipindi tofautitofauti, nilianza na Goma la Uswazi, ilikuwa
mara moja kwa wiki ambayo
ni Jumamosi tu.

“Wakaniongezea na Jumapili kisha baadae ikawa Ijumaa hadi Jumatatu, walipoondoka kina Dida kwenda Wasafi, ikabidi nifanye pia na Mitikisiko ya Pwani ambacho ni kipindi cha Taarabu.

“Nikapewa kipindi cha Umbea CCTV Camera, baadae nikawa nafanya na kipindi cha burudani ambacho alikuwa anafanya Idris wa Kitaa, Bongo.Com. Baadae nikaenda digital nikapewa kipindi cha Uswazi Macho kwa Macho.

 

MCHONGO WA CHUO VIPI?
“Nimesoma uandishi wa
habari ngazi ya cheti, ila diploma niliishia njiani.

 

KUHUSU MUZIKI WA SINGELI
“Msanii Young
Yuda ndiye aliyenifanya nipende singeli, Msaga Sumu na kaka yangu mkubwa pia.

 

KUHUSU MANARA
“Manara (Haji,
msemaji wa Yanga) ni mwalimu kwangu, nimejifunza vingi kutoka kwake, nilikuwa najifunza namna
ambavyo alikuwa
anapambana na watu wanaoichafua Simba.

 

ULIJISIKIAJE KUWA MC SIMBA DAY?
“Ilikuwa ni siku ya
kumbukumbu kwangu, kwa sababu sikutegemea mapokezi ya mashabiki ikiwemo kuwasha taa na
kusimama kwa kauli yangu
juu ya kumpokea Emmanuel Okwi.


“Nilipata pongezi nyingi
sana, kutoka kwa watu mashuhuri, waandishi wakubwa na viongozi wa serikalini. Ndiyo nilipata fedha lakini haikuwa kitu juu ya heshima kubwa niliyopata ya kuwahutubia watu zaidi ya 60 pale kwa Mkapa.

 

YEYE SIYO MHAMASISHAJI
“Niliweke sawa hili,
mimi siyo mhamasishaji, ila bado ni shabiki wa kawaida kama walivyo wengine. Ile
siku ilibidi kuzungumza ili
kuamsha morali kwa sababu palikuwa kama pamepoa,” anamaliza K Mziwanda.

Leave A Reply