The House of Favourite Newspapers

Kababu za Mayai na Nyama ya Kusaga

0

Na Gladness Mallya | RISASI JUMAMOSI | MAPISHI

NI wiki nyingine tena mpenzi msomaji tunakutana tena katika safu hii ya Mapishi ya Leo ambapo tunajifunza jinsi ya kuandaa kababu za mayai na nyama ya kusaga, ungana nami.

MAHITAJI

  • Nyama ya kusaga (kiasi unachotaka)
  • Mayai 5
  • Vipande vya mikate
  • Chumvi kiasi
  • Pilipili manga nusu kijiko cha chai
  • Pilipili nzima iliyosagwa nusu kijiko cha chai
  • Ndimu kipande
  • Mafuta ya kupikia
  • Mayai 2 ya kuchomea kababu
  • Bizari iliyosagwa
  • Vitunguu swaumu na tangawizi ya kusaga

JINSI YA KUPIKA
– Chemsha mayai mpaka yaive vizuri na uyamenye
– Chemsha nyama weka ndimu na chumvi.
-Ikikauka ichanganye na viungo vyote mpaka ichanganyike vizuri.

-Weka vipande vya mkate ambavyo unatakiwa uvivuruge kwa kuvishikia kwa maji kidogokidogo
-Vunja yai moja na uchanganye kwenye mchanganyiko wa nyama.
-Fanya mviringo na uweke kishimo cha kuweka yai ulilochemsha.

-Lifunge ndani vizuri yai kwenye nyama lisionekane.
-Piga yai kwenye kibakuli na uchovye mviringo kisha anza kuzikaanga ndani ya mafuta ambayo tayari yana moto.
-Ikiiva itoe na uiweke kwenye chujio kuchuja mafuta na itakuwa tayari kwa kula.

Leave A Reply