KESI ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwanadishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera, jana Februari 11, 2020 iliendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo upande wa mashtaka uliiomba kukutana na Kabendera kwa mazungumzo binafsi.
Uamzi huo ulifikiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Janeth Mtega, baada ya Wakili Mkuu wa Serikali, Faraja Nchimbi, kuwasilisha ombi hilo kwa lengo la wao kukutana na mshtakiwa na kukamilisha majadiliano ili kumaliza kesi hiyo.
Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu, ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na utakatishaji wa fedha zaidi ya shilingi milioni 170. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 17, mwaka huu itakapotajwa tena.