Kabendera Apooza, Mahakama Yatoa Maelekezo – Video

KESI inayomkabili mwanahabari Erick Kabendera imeahirishwa hadi Septemba 18, mwaka huu, ambapo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Augustine Rwizile, amemuagiza mtuhumiwa kuja kuieleza mahakama kile kitakachoendelea kuhusu afya yake.

 

Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo leo Septemba 12 kwa lengo la kutajwa, ambapo wakili wa upande wa serikali, Wankyo Simon, aliiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

 

Wakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo, Jebra Kambole, ameiambia mahakama kuwa  mteja wao bado anaumwa  mguu wa upande wa kulia kwa kuwa umepooza na kushindwa kutembea vizuri.

 

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu, ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na utakatishaji wa fedha zaidi ya Shilingi milioni 173.

 

Kwa mujibu wa mashtaka yanayomkabili, anadaiwa kuyatekeleza hayo kati ya  Januari 2015 na Julai mwaka huu, jijini Dar es Salaam,  makosa hayo yote yakiwa hayana dhamana hivyo ataendelea kusota rumande.


Loading...

Toa comment