The House of Favourite Newspapers

Kabila la Wala Watu-16

0

Wakati anatueleza hayo mara tukasikia sauti kali kutoka kwenye kichaka kilichokuwa karibu na pale tulipokuwa

MAKALA: ELVAN STAMBULI NA MTANDAO | UWAZI

Wiki iliyopita tulieleza jinsi Wamisionari wa Kidachi walivyoingia katika Kisiwa cha New Papua Guinea ili kueneza dini wakiwa na imani kwamba jamii ya huko itaacha tabia ya kula nyama za watu. Endelea…

WAMISIONARI walijitolea kuingia katika Visiwa vya Papua New Guinea ili kuwaelekeza mema makabila ya nchi hiyo ambayo yanakula nyama za watu.

Japokuwa kazi hiyo iliwafanya Wamisionari hao Wazungu baadhi yao kuuawa na kuliwa nyama zao lakini hawakukata tamaa, walijitoa kwa kuingia katika nchi hiyo na kuwafundisha ustaarabu watu wa huko.

Mzungu mmoja Mmisionari aliyekuwa na mwandishi wa habari walisimulia jinsi walivyokoswakoswa kuliwa na Wakorowai, moja ya kabila lililokithiri kwa kula nyama za watu katika visiwa hivyo.

Mwandishi Paul Ruffaele wa Jarida la Smithsonian anaeleza jinsi walivyoponea tundu la sindano katika safari yao kwenye visiwa hivyo hatari kwa wageni.

“Tulikuwa tuna nia ya kukutana na Kabila la Wakorowai wanaosifika kula watu. Tuliambiwa ili kwenda huko njia rahisi ni kwa kutumia mtumbwi. Hata hivyo, tulionywa sana kwamba ni hatari kwenda katika vijiji vya makabila hayo.

“Tuliambiwa mto ambao ungeweza kutufikisha katika vijiji vya makabila hayo ni Mto Ndeiram Kabur, hivyo walitupatia mwongozaji maarufu wa shughuli hiyo aitwae Kornelius Kembaren ambaye wageni wengi walikuwa wakimtumia kwa sababu alikuwa anajua lugha ya wenyeji na Kiingereza.

“Tulichukua mtumbwi na wapagazi wanne ambao nao walikuwa na makasia kwa ajili ya kusukuma mtumbwi kwenye maji ambao ulikuwa ndiyo usafiri wetu. Safari ilianza huku tukiwa na biskuti na maji. Baada ya mwendo mrefu giza lilianza kuingia huku tukiufuata mto ambao haukuwa na maji yanayokimbia sana.

“Nilikuwa na imani kwamba wakati wowote tunaweza kuweka kambi, wazo likanijia kwamba kama tutaweka kambi, tutakuwa salama kweli? Muongozaji wetu alituambia tusiwe na hofu kwa sababu amekuwa akiwaongoza wageni kwenye msitu huo kwa miaka 13,” alisema Kembaren.

Hata hivyo, alisema katika safari zote hizo watu wa Kabila la Wakorowai si wazuri kwa sababu wamekuwa wakitishia kuua wageni wanaoingia katika himaya zao. Kornelius alisema makabila ya huko hayana imani na Wazungu na huwa hawapendi kuwaangalia na mara nyingi wageni wamewapachika majina kwa kuwaita jina la Laleo wakiwa na maana kwamba ni mizimu au majini (Ghost- Demons).

Wakati anatueleza hayo mara tukasikia sauti kali kutoka kwenye kichaka kilichokuwa karibu na pale tulipokuwa.

“Nilishituka sana kumuona pande la mtu akiwa amesimama kando ya mto huku akiweka sawa mshale wake kwenye upinde. Nilijua sasa atakuwa anatumaliza kwa kutuchoma kwa mishale.

“Alituamrisha kupeleka mtumbwi wetu alikokuwa kwa mujibu wa mwongozaji wetu. Alikuwa akionekana kuwa ni mtu katili asiyependa masihara na hatukuwa na uwezo wa kumtoroka kwani kufanya hivyo kungemfanya atupige mishale.

“Mwongozaji wetu, Kembaren aliwaamuru wale vijana waliokuwa wakipiga makasia kusimamisha mtumbwi, mtu yule wa Kabila la Korowai alipotukaribia niligundua kuwa alikuwa uchi wa nyama.

“Alituamuru kushuka kwenye mtumbwi na kumfuata alipo. “Hatujaja huku kukudhuru,” alisema yule mwongozaji wetu kwa Lugha ya Bahasa Indonesia na kutafsiriwa kwa lugha ya Korowai na mmoja wapiga makasia kwenye mtumbwi wetu. “Tumekuja kwa amani,” aliongeza.

Mwandishi Paul anasema fikra zilimpeleka kwenye kumbukumbu zake kwamba watu hao ni wala watu na alikumbuka jinsi alivyosoma kwamba watu hao ambao wanaitwa ni wa Fiji wamekuwa wakila nyama za watu hasa Wazungu kama wao tangu karne ya 19.

Wakowai wanaishi Kusini Mashariki mwa kisiwa hicho cha Papua New Guinea. Hatukuthubutu kuwaeleza kuwa sisi ni wana habari kwa sababu walikuwa wakiwachukia sana watu wa habari kutokana na kufichua unyama wao badala yake tuliwaambia kuwa sisi ni watalii.

Kabla ya kufika katika kijiji hicho ambacho sasa Paul na wenzake walikuwa ni mateka, waliwahi kutembelea mji uitwao Jayapura nchini humo ambao una wakazi wanaokadiriwa kufikia 200,000, mji ambao upo Kaskazini Mashariki mwa visiwa hivyo.

Je, kilifuatia nini? Usikose kusoma habari hii ya kabila la wala watu wiki ijayo.

Leave A Reply