The House of Favourite Newspapers

Kabila la Wala Watu-17

0

Mchungaji Johannes Veldhuizen, Mdachi aliyepania…

ELVAN STAMBULI NA MTANDAO | UWAZI

MWONGOZA watalii, Kornelius Kembaren aliyekuwa anawaongoza waandishi Paul Ruffael katika vijiji vya Kisiwa cha Papua New Guinea wiki iliyopita tuliona jinsi walivyotekwa na watu wa kabila la wala nyama za watu, waitwao Wakorowai, endelea…

Ni ukweli ulio wazi kwamba Wakorowai wana uelewa mdogo sana kuhusu dunia kwa ujumla, wanachokijua wao ni kuhusu vijiji na jamii zao tu.

Ukatili wa kula nyama za watu siyo kwamba wanawafanyia wageni kama hao Wazungu tu bali pia wanatendeana wao kwa wao.

Inaelezwa kwamba wanaume wachawi ambao wao huwaita Khakhua kwa lugha ya Kikorowai, wameliwa sana baada ya kutuhumiwa kuwa ni wachawi.

Wanaamini wachawi wamekula sana nyama za wenzao, hivyo wazee wa kimila wakithibitisha kwamba fulani ni mchawi basi nao huamua kumla mwanaume au mchawi yeyote anayekamatwa.

Kwa wasiokijua kisiwa hiki cha Papua New Guinea, ni kwamba ni cha pili kwa ukubwa duniani baada ya kile cha Greenland. Kuna milima na ardhi nzuri kwa ustawi wa kila aina ya mazao yanayolimwa katika nchi yenye misitu minene inayopata mvua nyingi kwa mwaka.

“Muongozaji wetu, bwana Kembaren, 46, ni mtu wa Sumatra aliyefika katika kisiwa hicho miaka 16 iliyopita na alitembelea eneo la Wakorowai wala watu kwa mara ya kwanza mwaka 1993.

”Baada ya kukaa kipindi kirefu namna hiyo katika nchi hiyo, Kembaren alijua lugha nyingi za wenyeji wa nchi hiyo,” alisema mwandishi Paul.

Wamisionari wa Kidachi walioingia rasmi katika visiwa hivyo mwaka 1970 wamechangia sana kuwastaarabisha Wakorowai na jamii nyingine katika nchi hiyo ambayo ni hatari kuishi watu hasa Wazungu ambao vijiji vya Wakorowai Wazungu hao waliviita Jehanam ya Kusini kutokana na tabia ya wenyeji ya kufanya nyama za watu ni supu.

Muongoza watalii au watafiti Kembaren alikuwa mara kwa mara akiwaonesha Paul na wenzake ramani za kisiwa hicho na maeneo ambayo ni hatari, yaani yale ambayo watu huliwa sana na watu wa jamii za huko za wala minofu ya watu.

Mchungaji Johannes Veldhuizen, Mdachi aliyepania kueneza kanisa katika kisiwa hicho alikuwa miongoni mwa Wazungu waliojitoa kuingia katika visiwa hivyo kueneza Ukristo.

Wakorowai walikuwa na imani za kizamani kwamba milima mirefu ilikuwa na miungu ambayo ilikuwa ni tishio kwao kwa sababu waliamini wakikiuka maadili, basi miungu hao wataleta tetemeko la ardhi la kuwaua.

“Kwa hiyo tukiwa na wala watu hao tulikuwa na tahadhari kubwa katika jitihada zetu za kuwabadili tabia,” alisema mchungaji mwingine aitwaye Gerrit van Enk, Mdachi aliyewahi kuandika kitabu kiitwacho The Korowai of Irian Jaya, kinachoeleza tabia ya wala watu hao.

Mchungaji huyo alisema ni hatari sana kuishi na watu wa kisiwa hicho kwa sababu wanaweza kugeuka wakati wowote na kukufanya kitoweo.

Mchungaji huyo anasema kwa jinsi nchi hiyo ilivyo hatari kwa wageni, hata polisi na watabibu wanaogopa kwenda ndani zaidi ya misitu minene iliyomo kwenye kisiwa hicho kwa kuhofia kuliwa na Wakorowai.

“Kuingia katika eneo au utawala wa makabila hayo ya wala watu ni sawa na kuingia katika shimo refu la maji, ambalo usalama wa kutoka hai unakuwa mashakani,” alisema.

Hata hivyo, mchungaji huyo anasema licha ya sehemu kubwa waliyokuwa wanapita kuwa na misitu minene ilikuwa inapendeza kwa jinsi ilivyokuwa na wanyama wengi na sauti za kuvutia za ndege kama kasuku.

Lakini anasema wakati wanapita katikati ya misitu ya Wakorowai walikuwa wakikutana na nyoka hatari pamoja na buibui wakubwa (giant spiders) na vijidudu vidogovidogo vinavyosababisha maradhi ya ngozi yaani lethal microbes.

Mito mingi ambayo ipo katika maeneo ya wenyeji yamewekwa madaraja ya kienyeji, yaani magogo marefu kutokana na miti kustawi kwani kisiwa hupata mvua nyingi inayofikia inchi 200 kwa mwaka.

Kwa ujumla wamisionari wa Kidachi walikuwa na roho ngumu kwa sababu sehemu kubwa ya safari zao katika visiwa hivyo, walikuwa wakitembea kwa miguu na masanduku yao yalikuwa yakibebwa na wabagazi au makuli waliokuwa pekupeku ( barefoot porters).

Hata hivyo, wenyeji hao walikuwa wepesi kwa kutembea kwenye tope kwani sehemu nyingi ambazo Wazungu hao walikuwa wakipita zilikuwa na matope.

Paul anasema wakati wanazidi kuchanja mbuga kuelekea ndani zaidi ya misitu huku yule Mkorowai mmoja aliyewaibua kwenye mto akiwa mbele, mawazo yake yalikuwa kama watafika salama huko walikopelekwa kwa sababu walikuwa hawakujui.

“Baada ya mwendo mrefu, giza lilianza kuingia lakini kwa mbele tuliona mwanga, nilihisi kwamba ni kijiji kilichoundwa na wamisionari, “Tutalala pale,” alisema Kembaren lakini akili na mawazo ya Paul yalikuwa, Je, kile kijiji siyo cha wala watu?

Fuatililia Jumanne ijayo.

Leave A Reply