The House of Favourite Newspapers

Kabila la Wala Watu, Sehemu ya 10

Kabila la wala watu la Karowai visiwa vya Papua New Guinea.

TULIISHIA wiki iliyopita kuelezea jinsi Wazungu waandishi wa habari wa Uingereza walivyojikuta wakiwa chini ya kabila hilo la wala watu la Karowai kutoka katika visiwa vya Papua New Guinea. Tulieleza kwamba kabila hili lina taratibu moja, kwamba kama mwanaume anakamatwa kwa kujihusisha na uchawi, adhabu yake huwa kuliwa nyama yake, kitendo hicho wenyewe hukiita khakhua.   

Endelea:

WAINGEREZA hao walikamatwa baada ya kufika moja ya kijiji katika kisiwa hicho kiitwacho Wamena. Baadaye wote wakawa kama mateka na walipelekwa katika kijiji hicho na baada ya muda mfupi, ngoma ilipigwa na watu wakakusanyika. Wazungu wale wakajua kwamba ile ngoma ilipigwa kwa nia ya kuwakusanya wanakijiji ili kuja kushuhudia ujio wao pale kijijini.

Baada ya hotuba fupi kutoka kwa kiongozi wao, alitoa amri fulani na mtu mmoja mzee akaingia katika moja ya vibanda vilivyozunguka eneo walilokuwepo: “Hatukujua anafuata nini ndani ya kibanda kile, nilijaribu kuangalia watu wale waliokuwa vifua wazi, wa kike na wa kiume, ikatolewa maiti ya chifu wao aliyekaushwa kwa moto ili dua maalum lifanyike. Baadaye ngoma ilipigwa na wenyeji walikusanyika kuwashuhudia Wazungu hao, kiongozi wao alitumia nafasi hiyo kuwahutubia.

Hata hivyo, mwandishi Mwingereza aliyeandika habari hii alisema hakuwa anaelewa kile alichokuwa akisema kiongozi yule wa kimila. Kwa jinsi wananchi wenyeji wa kijiji hicho cha wala watu walivyokuwa wakishangilia hotuba ya yule chifu wao huku akiigusagusa ile maiti ya mtu aliyekaushwa, hofu iliwajaa Waingereza wale kwamba labda hotuba ile ilikuwa ni ya kufurahia minofu yao.

Kabila la wala watu

Hata hivyo, yule mkalimani wao Kembareni mara kwa mara alikuwa akiwapa moyo kwa kuwaambia kwamba watulie na wasiffanye jambo lolote baya. A n a s e m a walijiona wameshakuwa mateka na kwa jinsi vijana wa kabila hilo walivyokuwa wamepandwa mori walijua mwisho wao wa kuishi hapa duniani uliwadia, hali ilikuwa siyo shwari kama alivyokuwa akiwahakikishia mkalimani wao. Wapenzi wawili walisimulia jinsi walivyopatwa na wasiwasi baada ya kutekwa nyara na watu hao.

Brit Matthew Iovane na mwanamke wa Kimarekani Michelle Clemens, wote wakiwa na umri wa miakia 31, nao wanasema kuwa waliponea chupuchupu kuliwa. Waliogopa zaidi baada ya kuamriwa wote waliotekwa kufungwa macho;  hapo wakajua saa yao ya kifo ilifika kwani waliamriwa kwenda porini huku wakilindwa na wala watu hao. Matthew aliiambia Channel 4 ya Uingereza kwamba walipigwa kikatili sana na watu hao walipojaribu kuwatoroka.

“Tulikuwa tunaona kama masihara kuhusu wala watu hao wa Papua New Guinea lakini huwezi kucheka ukiwa mbele yao mwituni. Wengi walikuwa wamejipaka rangi miili yao, wakatukaribia na kufanya mduara kutuzunguka.

“Walitumia T-shirt (fulana) zetu kutufunga machoni, nilijiambia kimoyomoyo kwamba hawa wametuweka kweye orodha yao ya mlo (menu) ya siku hiyo, nilitetemeka sana,” alisema Matthew.

“Nilifikiria kwamba kama Napata mwanya kabla ya kuuawa, nitoroke,” aliongeza. Habari za kuliwa watu katika Kisiwa cha Papua New Guinea zilikuwa zinasikika hata mwaka 2012 kwamba wenyeji walikuwa wakitimiza mambo ya kimila.

Bibi wa kabila la wala watu

Kutekwa kwa watu wao mwaka huo kuliifanya ofisi ya Ubalozi wa Uingereza nchini humo kutoa tamko kwamba ni kweli watu hao wamepotea na ikasema;“ Jambo hilo tunachukulia kwa kipaumbele kikubwa.”

Matthew anasema nia yao ilikuwa kwenda kwenye mji wa Kokoda ambao upo maili 60 ambako kunatajwa kuwa ndipo walipo watu wasiostaarabika katika dunia hii. “Chakushangaza ni kwamba njiani wanavijiji walikuwa wakitushangilia na kuturushia maua na miti ya kijani tukiamini kwamba ni kutusalimia, kumbe labda walikuwa wakitushangilia kwa kuona kuwa wamepata nyama, “ alisema Matthew.

Alisema baada ya mwendo wa saa moja porini, wanakijiji hao waliwazunguka wengine wakiwa nyuma yao, hapo wakajua kwamba walikuwa kwenye hatari kubwa ya kuuawa. “Mmoja kati ya wala watu wale aliyekuwa amevaa kinyago usoni akanisogelea kisha kunisukuma, nilianguka na nilikuwa na wasiwasi mkubwa kwamba sasa ananimaliza kwa sababu alikuwa na mkuki mkononi,” alisema Matthew.

Je, nini kiliendelea? Fuatilia Jumanne ijayo

Comments are closed.