The House of Favourite Newspapers

Kabila Linalohusudu Vitambi Linalotembea Utupu-2

0

 

Wiki iliyopita tuliona jinsi Wabodi wanavyoishi wakiwa na tabia tofauti na jamii zingine za Kiafrika katika nchi ya Ethiopia kwenye Bonde la Mto Omo wanamoishi. Moja ya tabia ya ajabu kwa wanaume ni ya kutembea wakiwa watupu kama walivyozaliwa, hali inayoshangaza wengi, Endelea:

WABODI kwa kawaida ni wafugaji na wanaishi na mifugo yao ambayo ina thamani kubwa kwao kwani ndiyo inayotumika pia wakati mwanaume anapotaka kuoa. Hutumika kwa kutoa mahari.

 

Lakini kabila hili hutumia ardhi kwa kulima mtama kando kando ya bonde la Mto Omo na zao hilo ndilo kuu kwa kabila hilo.

Ng’ombe pia hutumika wakati wa kutoa jina kwa mtoto mchanga aliyezaliwa. Ikiwa mtoto huyo atapewa jina la babu, bibi, baba yake mdogo au mkubwa, shangazi, mwenye jina hupewa mfungo, kama vile ng’ombe au mbuzi kama heshima kwa jina lake kutumika na familia fulani hata kama watu hao ni wa ukoo mmoja.

 

 

Mifugo yao wakati wa kupelekwa kwa mhusika huchaguliwa yule ng’ombe au mbuzi aliyenenepa vizuri na hupakwa rangi mbalimbali na hufanywa sherehe maalum katika familia husika.

Wanawake hukaa ndani na mtoto mchanga na kundi la familia hutoka wakiwa na ng’ombe au mbuzi na kwenda kwa mwenye jina huku wote waliohusika na msafara huo huwa wamevaa ngozi.

Mtoto mchanga pia huwekwa kwenye ngozi ya ng’ombe ambayo ni maalum kwani hutengenezwa na kuwa laini baada ya kuhifadhiwa sehemu huku ikiwa imelowekwa na aina fulani ya miti ambayo huilainisha.

 

Ikitolewa na kukaushwa huwa ni ngozi laini ambayo haiwezi kumuumiza mtoto lakini pia huweza kutumika kwa kumbebea mtoto kama mama yake atataka kufanya hivyo.

Mwenye jina akikabidhiwa ng’ombe au mbuzi, hufurahi na hutoka nyumbani kwake na kwenda alipowekwa mtoto mchanga, akifika ndani, humchukua na kumwambia kwamba kuanzia wakati huo atakuwa anaitwa jina fulani (lake), hapo hulipuka vigelegele kutoka kwa akina mama ambao walikuwa na mtoto.

 

Nje ya nyumba kunakuwa na sherehe kubwa kwa watu kucheza ngoma na kunywa pombe, hali hiyo hudumu kwa siku nzima kwani mifugo mara nyingi kwa siku hiyo hupelekwa malishoni na vijana huku wazee wakiachwa wakishughulikia sherehe hiyo.

Kabila wa Wabodi wanafanana kwa tabia na kabila lingine katika maeneo hayo linaloitwa Wamursi, nao wanapotaka kumpa jina mtoto mchanga hufanya kama wenzao.

 

ELVAN STAMBULI NA MTANDAO | UWAZI

================================================

Nishushe Dar Live: Roma, Stamina Waweka Historia Dar Live (Pichaz + Videos)

Leave A Reply