Kaburi la Ballali kufukuliwa

Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Daudi Timoth Ballali

HII mpya! Kuna madai kwamba, kaburi la aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Daudi Timoth Ballali lililopo Makaburi ya Gate of Haeven (Geti la Mbinguni) Eneo Na. 6, Ploti Na. 241, Safu Na. 17 huko Maryland nchini Marekani lipo mbioni kufukuliwa ili kuwezesha vipimo vya vinasaba (DNA) kutumika kwa lengo la kubaini ukweli wa kifo chake, Ijumaa limeelezwa.

Gharama ya jumla ya kuwepo kwa kaburi hilo ambalo safu yake imepewa jina la Jesus In The Temple (Yesu Hekaluni) ni Dola za Marekani 4,800 (zaidi ya Sh. milioni 9 za Tanzania).
Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa Ballali aishiye Bongo, familia inaona ni vema kutimizwa kwa ombi hilo kwa vile manenomaneno kuhusu ‘Ballali kafa au hajafa?’ hayajawahi kufunga breki tangu tangazo la kifo chake, Mei, mwaka 2008.

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.

TWENDE PAMOJA

“Nadhani sisi familia hatuna umoja. Wengine waoga, wengine majasiri. Lakini kwa sababu hata sisi hatukuwahi kwenda Marekani kumzika ndugu yetu (Ballali), hivyo ili na sisi tuwe na amani na kujua moja, tumetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwasiliana na Marekani kwa lengo la kulifukua kaburi lake na kuutoa mwili.

“Hilo ni moja. Pili, mwili huo upimwe DNA ili kubaini kama aliyezikwa ni Ballali? Hili zoezi halitatusaidia sisi tu kama familia, lakini hata serikali yenyewe itakuwa na faida maana maneno yamekuwa mengi sana. Tumeshaandaa utaratibu wa kuonana na serikali kwa ajili ya kupanga hili,” alisema ndugu huyo akisisitiza kusitiriwa kwa jina lake.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe

BALLALI FEKI AUMIZA KICHWA

Ndugu huyo aliendelea kusema kuwa, tangu kifo cha Ballali, Mei, mwaka huo, Desemba posti ya kwanza ya mtu aliyejiita Ballali ilitupiwa kwenye mitandao ya kijamii akisema amekumbuka nyumbani Tanzania.

“Tangu wakati huo, mtu huyo amekuwa akitupia maneno ya kushutumu kwamba yeye amefariki dunia. Hata vyombo vya habari vya Tanzania vilipotembelea Marekani mwaka jana na kuthibitisha kifo cha mchumi huyo kwa kuliona kaburi lake, mtu huyo alisema anavishangaa vyombo hivyo kwa vile yeye yu hai.“Ndiyo maana tunataka kaburi kufukuliwa, mwili utolewe na kufanyiwa vipimo mara moja ili kuondoa utata huu,” alidai ndugu huyo.

WATOTO WA BALLALI KUTUA BONGO

Ndugu huyo alizidi kuweka bayana kuwa, habari alizonazo ni kwamba, watoto wawili wa marehemu ambao alizaa na mwanamke, raia wa Marekani wapo kwenye mchakato wa kutua Bongo wakati wowote kwa mambo mawili makuu.
“Nasikia wanakuja. Lakini lengo la ujio wao ni kusema wanachokifahamu kuhusu kifo cha baba yao. Sasa sijajua watasema alifariki dunia au hajafariki dunia! Hiyo ni siri yao nzito, ipo mioyoni mwao.

“Lakini nijuavyo mimi kilio kikubwa cha hawa watoto mwaka ule wa tangazo la kifo kilikuwa ni kukosa kuiona sura ya baba yao wakati wa kuuaga mwili mpaka unaingizwa kaburini kwa mazishi.

“Kingine wanafuatilia hisa. Baba yao aliweka hisa kiasi cha shilingi bilioni 3 kwenye kampuni moja ya bia Tanzania. Sasa kutokana na kusuasua kwa maelezo yasiyonyooka kuhusu faida na hasara za hisa zile, ndiyo maana wanakuja. Nasikia tayari wana mwanasheria kwa ajili ya kupata haki yao hiyo,” kilimalizia chanzo hicho.

LOWASSA AOMBWA KUMLETA BALLALI

Katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, mgombea wa urais kwa ‘leseni’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amekuwa akiombwa na wapiga kura wake kumleta Ballali mara tu atakapoingia ikulu, jambo ambalo alikubaliana nalo.

Lakini naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameibuka na kuonesha kushangazwa na suala hilo kwani anachokijua kama waziri mwenye dhamana ni kwamba Ballali alifariki dunia mwaka 2008

.JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Loading...

Toa comment