The House of Favourite Newspapers

Kabwili: Nitaipa Ubingwa Yanga

Ramadhani Kabwili.

LICHA ya baadhi ya mashabiki wa Yanga kutokuwa na imani na kipa wao Ramadhani Kabwili, mlinda mlango huyo amesisitiza kwamba yeye ndiye atakayewapa ubingwa.

 

Kabwili amejipatia umaarufu na nafasi ya kudakia katika kikosi cha Yanga baada ya kuondoka kwa kipa namba moja, Beno Kakolanya ambaye ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kuigomea timu hiyo kwa kudai maslahi.

 

Kabwili ameanza kuidakia timu hiyo tangu mzunguko wa kwanza wa ligi kuu mara baada ya kuondoka Beno huku akisaidiana na Klaus Kindoki ambaye amekuwa hapewi nafasi sana kutokana na kiwango chake kutoaminika.

 

“Nitajituma kwa moyo wote kuhakikisha timu yangu ya Yanga inatwaa ubingwa msimu huu kwa kuhakikisha naidakia ipasavyo. “Kwa upande wangu sina wasi na nafasi yangu hii niliyoipata ya kudaka kama kipa wa kutegemewa kwa sasa na kikubwa kwangu ni kuona naendelea kujituma ili kiwango changu kiendelee kuwa juu,” alisema Kabwili.

KHADIJA MNGWAI

Comments are closed.