Kada CCM asimulia alivyonusa kifo!

kada
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni mjumbe wa UVCCM-Mkoa wa Morogoro, Hery Francis Hoza akiugulia.

Makongoro Oging’ na Issa Mnaly

AJALI! Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni mjumbe wa UVCCM-Mkoa wa Morogoro, Hery Francis Hoza ,32, (pichani) amepata ajali mbaya katikati ya wiki iliyopita na kunusurika kifo.

Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Kibaha mkoani Pwani ambapo kada huyo alikuwa akitoka Morogoro kuelekea Dar es Salaam.

chamaAkisimulia alivyonusurika kifo hicho akiwa wodini katika Hospitali Teule ya Rufaa ya Tumbi alikolazwa, majeruhi huyo alisema:

“Ilikuwa saa tatu asubuhi nikiwa naendesha gari. Nilikuwa na rafiki yangu, Nicodemas Tambo ambaye yeye hakupata majeraha.

“Sehemu zote niliendesha vizuri na hata nilipofika Kibaha nilijua nimefika Dar tayari. Unajua dereva yeyote akifika Kibaha anaamini ameshamaliza safari. Lakini kumbe Mungu ana mipango yake na binadamu ana mipango yake.

“Tukiwa tunapita eneo hilo, ghafla mbele yetu lilitokea lori. Sikujua nini kilitokea, lakini ghafla wakati wa kupishana, nikasikia kishindo kikubwa sana. Kumbe ndiyo ilikuwa ajali na mimi niliumia kichwani kama unavyoniona hapa,” alisema Hoza.

Akaongeza: “Niliumia sana. Nililetwa hapa na kushonwa nyuzi 36 kichwani ila naendelea na matibabu. Lakini kusema kweli namshukuru sana Mungu kwa kuniponya kwani ilikuwa nife, maana mwenzangu alifanyiwa uchunguzi na hakupatikana na madhara yoyote hivyo aliruhusiwa kuendelea na safari ya kurudi Dar.”


Loading...

Toa comment