The House of Favourite Newspapers

Kada Hamis wa CCM Ajitolea Kuchangia Ujenzi wa Ofisi ya Chama Muheza

0

 

 

Hamisi Sadiki Rajabu ambaye ni Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Mwananchi wa Wilaya ya Muheza ameendelea kufanya maajabu kwa kuendelea kuchangia na kushiriki miradi ya kijamii na maendeleo wilayani humo.

 

Akiwa Muheza leo Jumamosi tarehe 25 Februari, 2023, Hamisi ameshiriki katika ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Nkumba pamoja na kutoa matofali 400 pamoja na mifuko 10 ya cement kwa ajili ya ujenzi huo. Vilevile Hamisi ametoa matofali 2,000 ya kuchoma kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Kata ya Kwemingoji wilayani humo.

 

 

Ushiriki na kuchangia kwake maendeleo katika Wilaya hiyo ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan. Mhe. Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanzania inajikomboa kiuchumi na hivyo kumshawishi Hamisi kujitoa kwa moyo wa dhati katika kushiriki na kuchangia miradi ya kijamii.

 

Hamisi ambaye kwa nyakati tofauti aligombea Uspika wa Bunge la Tanzania, Ubunge Jimbo la Muheza, pamoja na Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, amekuwa mfano wa kuigwa na wananchi wote wa Muheza wamekuwa wakimuongelea Hamisi kama kijana shujaa, mwenye ushawishi na maono, na aliye na dhamira ya dhati ya kuiona Muheza ikisonga mbele kimaendeleo.

 

Msemo wake wa ‘Muheza na mimi, mimi na Muheza’ wengi wanautafsiri kama utayari wa kivitendo katika kuipambania Muheza.

Leave A Reply