The House of Favourite Newspapers

Kadi Nyekundu za Ruvu Zamtoa Neno Mkwasa

0

KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kitendo cha wachezaji wake Juma Nyoso na mlinda mlango, Abdallah Rashid kupewa kadi nyekundu kimemvurugia mipango yake kwa michezo minne iliyosalia ambapo timu yake inatakiwa kupambana ili kujinasua na janga la kushuka daraja.

 

Kocha huyo ambaye amewahi kuifundisha timu ya taifa, Taifa Stars amesema baada ya wachezaji hao kupewa kadi hizo hana namna zaidi ya kuwaamini waliopo na kufanya nao kazi.

 

“Kiukweli tumefanya makosa na tuliadhibiwa na Simba kwani ukiangalia bao la kwanza ni kutokuwa makini na hata bao la pili wachezaji wangu walizubaa na tukafungwa, hivyo tutakwenda kujipanga ili tufanye vyema kwa michezo minne ambayo imebaki.

Katika mchezo wetu na Simba wachezaji wangu wawili walipata kadi nyekundu na kiukweli lazima niwe wazi kwamba wataniharibia mipango yangu kwenye timu kiujumla kwani ukiangalia Nyoso ni mchezaji mzoefu na hata golikipa wetu naye ndiye alikua namba moja lakini kwa sasa sina jinsi natakiwa kuwaamini waliopo ili wanifanyie kazi.

 

“Tuko katika vita kubwa kulingana na pointi tulizonazo lakini michezo minne yote tuliyonayo tunacheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani bila presha na mimi kama kocha nitachukua tahadhari zote kuhakikisha nainusuru timu yangu na janga la kucheza playoff au kushuka daraja.

Leave A Reply