The House of Favourite Newspapers
gunners X

KADINALI PENGO: “HAWA WALEVI, WANAPATA WAPI MUDA WA KULEWA SAA 3 -VIDEO


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema ili Roho Mtakatifu asibezwe na kusahaulika kuwa ni Mungu wa pili linahitajika kanisa linaloshirikiana na Serikali katika kuweka mazingira yanayotakiwa.

 

Ameyasema hayo leo Aprili 28, 2019 katika misa ya kumsimika Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Gervas Nyaisonga iliyofanyika katika viwanja vya Sokoine na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais John Magufuli.

Kulewa kabla saa tatu asubuhi kunahusisha tukio la wanafunzi wa Yesu kujazwa Roho Mtakatifu saa tatu asubuhi na kuanza kunena kwa lugha tofauti jambo ambalo liliwafanya watu kufikiri walikuwa wamelewa.

“Lakini ina maana kuwa mimi kama askofu mkuu siwezi kubeza shughuli inayofanywa na Serikali katika kuwapa vijana nidhamu na kufanya hivyo utakuwa unakwenda kinyume na Roho Mtakatifu.”

 

“Kwa sababu kazi iliyo njema na inayowapa vijana wetu nidhamu ya kutokulewa kabla ya saa 3 asubuhi ni ile inayowezekana tu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu neno hilo ni la muhimu kila mtu kulitambua,” amesema Pengo

“Mpokeeni na kumuenzi Roho Mtakatifu na ondoeni  dhambi. Ni dhambi peke yake inaweza kutupatia sababu ya kubaguana na kufanya yasiyofaa na yale yasiyo ya matendo,” amesema Pengo.

“HIYO SADAKA NILIYOIKUSANYA MKAIHESABU VIZURI, NILITAMANI NIWE PADRI” – JPM

Comments are closed.