KADINDA: WEMA AMEKUA, AJIONGOZE MWENYEWE
DAR ES SALAM: Aliyekuwa meneja wa mwigizaji Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi Bongo amefunguka kuwa kutoonekana muda mwingi na mlimbwende huyo haimaanisha hawana uhusiano mzuri bali amemwacha staa huyo ajiongoze mwenyewe kwani amekua.
Kadinda amesema kuwa Wema amekua hivyo kwa sasa anatakiwa ajiongoze mwenyewe kwa kutumia elimu yake aliyonayo kuendesha biashara zake.
“Unapokuwa na elimu naamini ni rahisi kufanikiwa kwenye vitu unavyofanya kwa kuwa changamoto utazichukulia katika hali chanya, hutakuwa mwepesi wa kukata tamaa, hivyo basi Wema ni mwanadada msomi na anaweza kufanya hivyo kwani amekua na sasa anatakiwa kujiongeza mwenyewe,” alisema Kadinda.
Akizungumzia mwenendo wa Wema kwa sasa, Kadinda alisema mwanadada huyo anamuona ametulia tofauti na awali ambapo alikuwa hakaukiwi matukio.
Stori: MWAMDISHI WETU, IJUMAA
Comments are closed.