The House of Favourite Newspapers

Kadja Nito: Mahaba anayonipa mume wangu sijutii kubadili dini! (+Video)

khadija-nito-2

MAMBO vipi mpenzi msomaji  wa Mpaka Home, kwetu mambo yanaendelea kuwa mazuri kwa sababu tunakupa kitu kilicho bora.

khadija-nito-3Wiki hii Mpaka Home ilitembelea nyumbani kwa mwanamuziki anayetamba na Kibao cha Maumivu,  Kadja Nito ambaye anaishi Mwenge jijini Dar, akiwa na mumewe Tresor, lakini kitu kikubwa kinachovutia nyumbani hapo ni aina ya maisha wanayoishi na mumewe huyo kwa sababu kila mmoja anaonyesha mapenzi ya dhati kwa mwenzake.

khadija-nito-4Tumezungumza naye vitu vingi, kuyajua yote twende pamoja hapa chini:

Nini kilimfanya kubadili dini kutoka Uislamu kwenda kwenye Ukristo na kuamua kuolewa?

khadija-nito-5“Unajua kwanza kabisa niliamini kuwa Mungu tunayemuamini ni mmoja lakini kikubwa nilimfuata mume wangu kwa kuwa nilimuona wazi ni mwanaume mwenye upendo wa dhati na wa kweli ambaye ananifaa kwenye maisha yangu na amenibadilisha kwa kiasi kikubwa mno.

khadija-nito-6Anasemaje mgogoro wake na wazazi wake kuhusu kubadilisha dini?

“Unajua kuna kitu naamini katika maisha kuwa  kuolewa ni jambo jema na ni heshima kubwa kwa wazazi wangu, najua pia hawakupendezwa na mimi kubadili dini lakini najua ipo siku wataelewa na haya yataisha na tutakuwa kama zamani kwa maana ningeweza kumpata mwenye dini yangu akawa hana upendo kama huu ninaoupata sasa kutoka kwa mume wangu na mwisho ndoa ikavunjika.

khadija-nito-7Nini anachopenda kufanya anapokuwa nyumbani?

“Huwezi amini tunapokuwa tumemaliza kazi zetu mbalimbali za hapa nyumbani, mimi na mume wangu vitu vingi tunafanya kwa kusaidiana. Tunapendana sana, tunatumia muda mwingi kusali na tunaamini katika kusali ndiyo vitu vingi vinafu-nguka katika maisha yetu.

khadija-nito-8Tofauti ya maisha ya ubachela na sasa kwe-nye ndoa ni ipi?

“Tofauti ipo kubwa sana, zamani nilikuwa naweza kutoka kwenda sehemu mbalimbali za starehe au kuwa na marafiki ambao wana mawazo mabaya lakini sasa hivi huwezi kunikuta kumbi zozote za starehe kwa sababu ya mwongozo mzuri kutoka kwa mume wangu na ukweli nafurahi sana nilivyo sasa.

khadija-nito-10Ni chakula gani anapenda kukipika au kumpikia mumewe?

“Mara nyingi napenda kupika vyakula mbalimbali lakini kikubwa napikaga chakula cha kabila la mume wangu yaani Kikongo, kinaitwa Sombe ambacho amenifundisha yeye kwa sababu mara nyingi huwa yeye ndiye yuko jikoni na hapo ndipo naangalia jinsi mume wangu alivyo na mapenzi ya kweli na kwake sijafuata pesa zaidi ya hayo mapenzi.

khadija-nito-12Vipi kuhusu kazi yake ya muziki na ndoa?   

“Hakuna shida kabisa ukizingatia mume wangu anaheshimu sana kazi yangu na mara nyingi sehemu ninazoenda kwa ajili ya muziki na yeye yupo ananiachia huru na vitu vyote hivyo naona naweza kuvimudu labda ningekuwa na mume mkorofi hapo ingekuwa ngumu kwangu.

khadija-nito-15Nini anachofurahia katika maisha yake?

“Ninachofurahi ni kumpata mume wa maisha yangu na mwenye upendo wa kweli, Ananidekeza ile mbaya. Naweza kusema huyu mume wangu ananichukulia kama mtoto kwa sababu vitu vingi anafanya yeye kuna wakati hataki nifanye kitu hata viatu navalishwa nitake nini tena!”

Kadja Nito: Kwa Mahaba Anayonipa Mume Wangu, Sijutii Kubadili Dini

Comments are closed.