The House of Favourite Newspapers

Kadjanito: Usupastaa siKazi rahisi

0

NitoKhadija Maige ‘Kadja Nito’.

Stori: Suzan Kayogela 

Mwanadada anayesumbua kwa sauti laini kwenye gemu ya Bongo Fleva, Khadija Maige ‘Kadja Nito’ amesema kuwa anatamani kuona anazidi kung’aa zaidi na kuwa supastaa wa kimataifa lakini si jambo rahisi kwa kuwa inahitaji kujipanga zaidi kuliko watu wanavyofikiria.

Akizungumza na Uwazi Showbiz, Kadja Nito amesema kuwa watu waelewe kuwa mazingira ndiyo mara nyingi husababisha msanii kuwa kimya kwa muda mrefu bila kutoa wimbo na si kama anafanya makusudi na kuongeza kuwa ili kuwa supastaa inahitaji nguvu ya ziada.

“Watu wafahamu kuwa supastaa siyo kazi rahisi, kila mmoja wetu anatamani afikie huko kwa kutoa nyimbo kali kila wakati, lakini mazingira ya muziki wetu  na soko linatufanya tusifikie malengo yetu kwa muda tuliojipangia,” alisema Kadja.

Leave A Reply