The House of Favourite Newspapers

Kagaigai: Wabunge Waliotimuliwa CUF, Mahakama Haijaamuru Warudishwe Bungeni

0
Kagaigai na Spika Ndugai.

KATIBU wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Stephen Kagaigai amekanusha taarifa zinazovumishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wabunge nane waliovuliwa ubunge baada ya kufukuzwa na chama cha wananchi CUF wamerejeshwa bungeni kwa amri ya mahakama.

 

Akitoa ufafanuzi huo kwenye ofisi za Bunge Dodoma, Kagaigai anasema mahakama imetoa uamuzi wa awali juu ya walalamikiwa wa shauri la wabunge hao ambao ni baraza la wadhamini na uongozi wa CUF kuwa wasitishe utekelezaji wa kuwafukuza uanachama na kutojadili uanachama wao hadi mahakama itakaposikiliza shauri lao la msingi.

 

Aidha, Kagaigai amesema nafasi za ubunge hao tayari zilijazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria, na wabunge waliopatikana kujaza nafasi hizo wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya kibunge ipasavyo.

 

Novemba 10,mwaka huu mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam ilitoa uamuzi wa awali katika shauri namba 479 la mwaka 2017 lililofunguliwa na waliokuwa wabunge nane wa CUF viti maalum uliotafsiriwa tofauti na baadhi ya watu kwa kudhani wabunge hao wamerejeshewa uanachama wao na hivyo wanarudi katika nafasi zao za ubunge.

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

VIDEO: Dk Shika Atamba Kutikisha Usiku wa 900 Itapendezaa

Leave A Reply