The House of Favourite Newspapers

Kagame: Kuna Fursa ya Amani DRC, Lakini Msukumo wa Nje na FDLR ni Vikwazo

Rais wa Rwanda, Paul Kagame

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amesema kuna fursa ya kufikiwa kwa makubaliano ya amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lakini akasisitiza kuwa chanzo kikuu cha mzozo huo ni msukumo kutoka nje ya nchi hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Kagame alieleza kuwa juhudi zozote za kutatua mzozo huo hazitaweza kufanikiwa bila kuhusisha kikamilifu suala la kundi la waasi la FDLR, ambalo mara kwa mara Rwanda imelilaumu kwa kuhatarisha usalama wa taifa lake.

“Hatua yoyote ya kweli ya kutatua mzozo wa DRC lazima ijumuishwe na suala la FDLR.”

Kagame pia aligusia juhudi za kidiplomasia zilizowahi kufanywa na aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, akisema kuwa Rwanda inaunga mkono maamuzi na jitihada hizo katika kutafuta suluhu ya kudumu.

“Rwanda inaunga mkono juhudi na maamuzi ya Trump kuhusu mgogoro wa DRC.”

Kwa mujibu wa Kagame, mgogoro huo unahitaji kutazamwa kwa upana wake wote, kwani unahusisha vipengele vya kisiasa, kiuchumi, na hasa msukumo wa nje, akimaanisha ushawishi au maslahi ya mataifa mengine katika eneo hilo.

  “Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unahusisha pande tatu: kisiasa, kiuchumi, na msukumo wa nje,” alisema.

Akihitimisha, Kagame aliahidi kwamba Rwanda itatimiza wajibu wake iwapo kutafikiwa makubaliano ya amani, lakini akasisitiza kuwa utekelezaji wa makubaliano yoyote ni jukumu la serikali ya DRC.

HISTORIA YA MWAKA MPYA WA KIISLAMU – IJUMAA ADHWEEM