Kagasheki; Magufuli ni jembe, awanasa wapinzani

DSC_2132

Khamis Sued Kagasheki.

MIAKA zaidi ya 14 iliyopita, siasa za Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera, hazikufikiria kama kuna mtu aliyeitwa Khamis Sued Kagasheki. Hata alipojitokeza, alionekana mgeni kwa wakazi wengi wa Bukoba.

Mwaka huu, Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli alimnadi Kagasheki na kumtaja kuwa ni mtu anayefaa kuwa mbunge kuliko wagombea wote lakini naye akamnadi mwakilishi huyo wa urais wa chama chake, kwamba ni jembe.

Kagasheki alipotangaza nia yake ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM kwa mara ya kwanza, alipata wakati mgumu wakati wa kampeni. Alihujumiwa hata na wana-CCM wenzake aliowategemea, kwani baadhi yao walivaa mashati ya kijani mchana na kuwa upande mwingine usiku.

01Kwa takriban miaka 14 sasa, siasa za Bukoba Mjini zimetawaliwa na ushabiki wa CCM chini ya Kagasheki na Chama cha Wananchi (CUF) ambacho hata hivyo kamanda wao aliyewaongoza kipindi cha 2000-2005, Wilfred Lwakatare aliamua kuachia jahazi na sasa yupo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kagasheki aliikuta Bukoba ikiwa na siasa za mgawanyiko, chuki na uhasama wa kiitikadi. Lakini aliingia kwa ahadi za maendeleo, lugha ya ushirikiano na upatanishi na uwakilishi usiojali itikadi.

Kwa baadhi ya wanaCCM waliomuunga mkono, hili lilikuwa tatizo; kwani wao walitaka awe kama wao, asicheke na wapinzani.

Kwa wapinzani hawa wa CUF miaka ya 2008, alionekana kama hajui siasa za chama tawala, kwani aliwakumbatia wapinzani badala ya kuwapinga, hivyo wakanasa. Imewachukua muda wakazi wa Bukoba kumzoea na sasa wamezoea staili yake ya siasa na utendaji wake.

“Jambo hili nimekuwa nalisema, tangu wakati wa kampeni na hata sasa, kwamba lengo langu ni kuwa mwakilishi wa wakazi wa Bukoba, si mwakilishi wa wanaCCM.

“Najua wakati wa kampeni huwa tunashindana, lakini baada ya matokeo na mimi kuwa mwakilishi wa wakazi wa Bukoba, kazi yangu huwa ni kutetea wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa….katika uwakilishi wangu sina cha itikadi,” anasema Kagasheki.
Msimamo huu umempatia Kagasheki mahali pa kuanzia kufanya siasa za Bukoba.

memgombanisha na baadhi ya wanaCCM wahafidhina katika jimbo lake lakini umempatia wafuasi wengi kutoka upande mwingine kwani ameonekana anafanya siasa za kiungwana zinazokubalika.

Anasisitiza kuwa siku zote anataka maendeleo ya Bukoba, si maendeleo ya vyama. Kwa sababu hiyo, leo hii Bukoba imekuwa tofauti kabisa na ilivyokuwa awali, na baadhi ya wakazi wamesahau tofauti zao za kiitikadi.

Kagasheki anawaonesha wana Bukoba kuwa wakati wa siasa chafu, kubaguana na kudidimia kielimu na kimaendeleo umepita. Anasema wakati uliopo ni wa wana Bukoba kuupiga vita umaskini kama anavyohamasisha Dk. Magufuli katika kampeni zake za kuwania urais.

Anasema wajibu wake ni kuwapatia wananchi wa Bukoba fursa ya kupiga hatua kimaisha kuwa na barabara nzuri, usafiri wa uhakika wa magari, meli na ndege – mambo ambayo hayajali itikadi za siasa kama alivyoahidi mgombea wa urais wa CCM, Dk. John Magufuli alipofanya mkutano wa kampeni mwaka huu.

Wapo waliompinga zama zile lakini sasa wanamuunga mkono kwa dhati, kama anavyosema Veronica Bashaija, mkazi wa Bukoba Mjini:

“Huyu bwana sasa tumemjua, na hata baadhi yetu tuliokuwa tunamkataa, sasa tunamkubali, ni mchapakazi kwelikweli.

“Kinachoonekana hapa ni kwamba tuna mwakilishi mwenye upeo mkubwa sana, asiyeendekeza siasa za kizamani, bali anapigwa vita na baadhi ya wanaopaswa kumsaidia, hasa ndani ya chama chake, wanaoona kwamba anawapiku kwa mawazo na mipango ya kisasa, na anatekeleza ahadi zake, huku haendekezi ubaguzi wa kisiasa kama alioukuta.”

Kutokana na mwelekeo mpya wa siasa shirikishi anaoujenga Kagasheki, wengi wanamuona kama daraja la kisiasa kati ya kambi za CCM, Chadema na CUF.
Katika kata 14 za jimbo hilo, hii ya kuvunja ukuta wa u-CCM na upinzani katika uwakilishi wake, ni moja ya sifa kubwa alizojizolea katika kipindi chote alichochaguliwa kuwakilisha jimbo hilo.

Lakini Kagasheki ana sifa ya ziada jimboni Bukoba. Alitoa ahadi nyingi wakati wa uchaguzi, ameshatekeleza nyingi katika kipindi kifupi. Ni ahadi zinazoonekana na kushikika.

Kwa mfano, aliwahi kuahidi kununua gari la wagonjwa, akalinunua na ni kwa wakazi wote wa Bukoba wanapouguliwa au wanapofiwa.

Popote walipo watafuatwa na kuhudumiwa bila gharama yoyote kutoka mifukoni mwao.
Sambamba na huduma hii ya usafiri, kama ni msiba, mbunge pia hutoa ubani kwa kila msiba unaohudumiwa na gari hilo.

Si katika shida tu, bali hata katika raha, zikiwamo ibada za kidini, mbunge huyo amekuwa akishirikiana na watu wa dini zote kwa namna mbalimbali.

Kwa mfano, wakati wa hija za Wakristo Wakatoliki Jimboni Bukoba kwenda Nyakijoga, Mugana, Kagasheki aliwahi kuweka utaratibu wa kuwapatia usafiri kwa kushirikiana na viongozi wao hadi Mugana, umbali wa kilometa 27 kutoka Bukoba mjini.

Balozi Kagesheki ameweza pia kutoa magodoro na vyandarua katika hospitali ya mkoa iliyomo jimboni mwake, huku pia akisaidia maandalizi ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bukoba katika eneo la Zamzani.

Kagasheki ameweza kumpeleka daktari wa macho kwa gharama zake Bukoba mjini ambapo wananchi 6,000 walipima macho na kupatiwa miwani.

Miongoni mwa mambo yanayozungumzwa mjini Bukoba kuhusu ushiriki wa Kagasheki katika suala la elimu ni misaada katika Kijiji cha Kibeta. Hapa kuna shule ambayo imekuwa na tatizo la kupigwa radi kila mara kwa miaka kadhaa.

Hatua aliyochukua mbunge huyo kwa haraka ni kugharamia ujenzi wa mtego wa radi na elimu kwa watoto ambao wazazi wao hawana uwezo.

Loading...

Toa comment