The House of Favourite Newspapers

Kagera: Moto Wateketeza Mabweni, Mwanafunzi Afariki Dunia

MWANAFUNZi  wa darasa la tano katika Shule ya Msingi St. Joseph Rutabo mkoani Kagera amefariki na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya mabweni mawili ya shule hiyo kuteketea usiku wa kuamkia leo.

Bweni hilo limeteketea leo Alhamisi Julai 26, 2018 huku mashuhuda wa tukio hilo wakisema viongozi wa wilaya hiyo wapo katika kikao na walimu kujadili tukio hilo.
Kwa mjibu wa Afisa elimu mkoa wa Kagera Aloyce Kamamba amesema mwanafunzi wa darasa la tano ameungua na kufariki hapohapo lakini wengine wanaendelea kupatiwa huduma,

Chanzo cha cha moto bado hakijajulikana huku jitihada za kuokoa na kuzima zikiendelea.
Endelea kufuatilia taarifa zetu kupitia mitandao ya Global Publishers ili kufahamu zaidi.

Comments are closed.