The House of Favourite Newspapers

Kagera Mpo Siriazi au Mnazuga?

LICHA ya dirisha dogo kufunguliwa lakini kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema hana mpango wa kusajili mchezaji yoyote katika usajili huu.

Katika dirisha lililopita kocha huyo aliweza kuongeza wachezaji wengi na hivyo amesema kipindi hiki hana mpango wa kuongeza mchezaji.

 

Mecky alisema kuwa kikosi chake kipo kamili zaidi anahitaji kujipanga zaidi na kuhakikisha wanapata matokeo katika mechi zao zijazo za ligi.

Kagera inatarajiwa kuvaana na Yanga mapema Novemba, 25 mwaka huu katika Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.

 

“Kwa sasa sina mpango wa kuongeza mchezaji katika dirisha hili labda itokee tu sababu wachezaji wangu wapo vizuri na zaidi nafanya tu marekebisho pale penye mapungufu.

“Na kwa sasa tunaendelea na maandalizi ilikuhakikisha tunashinda mechi zote ambazo zipo mbele yetu japo ushindani ni mkubwa kwa sasa,”alisema Mecky.

MARTHA MBOMA, SPORT XTRA | DSM

KISHINDO Cha ujio mpya wa HABARI ZA MICHEZO Global TV Online

Comments are closed.