The House of Favourite Newspapers

Kagera Sugar Wanaingia Jumatatu

KAGERA Sugar inaingia kambini Julai 23 mwaka huu, tayari kujiandaa na msimu ujao wa ligi Tanzania Bara.

 

Timu hiyo ambayo inamilikiwa na kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar cha mkoani Kagera pia itaingia kambini kufanya mazoezi ili kujiandaa na michuano ya kombe la FA.

 

Akizungumza na Championi kwa njia ya simu akiwa mkoani Kagera, Kocha mkuu wa Kagera, Mecky Maxime amesema kuwa, timu yake itangia kambini Julai 23 na watahakikisha msimu ujao wanafanya vizuri.

Stori: Abdallah Zalala | Championi Ijumaa

Comments are closed.