The House of Favourite Newspapers

KAGERE AFANYA YAKE, AWAPIGA MBILI KAVU JKT

Mambo mawili yaliyofungwa na Meddie Kagere katika dakika za 11 na 38 kipindi cha kwanza yameiwezesha Simba kung’ara kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania.

 

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, Simba ilimuazisha kiungo wake Mghana, James Kotei ambaye alikuwa anatumikia adhabu kufuatia kumpiga Gadiel Michael katika mechi ya mwisho iliyowakutanisha watani wa jadi.

 

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuikimbiza Azam FC iliyo na pointi 27 kileleni kwa kufikisha alama 26.

Licha ya ushindi huo, Kocha Patrick Aussems ameulalamikia Uwanja wa Mkwakwani kuwa si rafiki kwa kuchezea na akiomba kama kuna uwezekano uweze kufanyiwa ukarabati.

NA MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.