Kagere Afunga Mabao 58 Bongo

MSHAMBULIAJI namba tatu ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21, Meddie Kagere ametupia jumla ya mabao 58 ndani ya ardhi ya Bongo kwenye Ligi Kuu Bara.


Raia
huyo wa Rwanda amekuwa na ushkaji mkubwa wa kucheka na nyavu pale anapopata nafasi jambo ambalo limekuwa likimbeba mara kwa mara.

 

Msimu wake wa kwanza 2018/19 alipojiunga na Simba akitokea Klabu ya Gor Mahia ya Kenya alitupia mabao 23 na ule wa pili wa 2019/20 alitupia mabao 22 katika misimu miwili mfululizo alisepa na tuzo ya kiatu bora.

 

Msimu wa 2020/21 Kagere ametupia mabao 13 akiwa nafasi ya tatu ndani ya Simba kwa sababu kinara ni John Bocco mwenye mabao 16 anafuatia Chris Mugalu mwenye mabao 15.

 

Kwa misimu mitatu ambayo amecheza nyota huyo ameweza kufunga jumla ya mabao 58 ikiwa ni rekodi yake bora akiwa na Simba kwa kuwa muda wote wa misimu mitatu alikuwa akinyanyua taji la Ligi Kuu Bara.

STORI: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam3403
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment