The House of Favourite Newspapers

Kagere Awaandalia Azam Kitu Mbaya

KATIKA kuhakikisha Simba inaendelea kufanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu Bara, mshambuliaji wa timu hiyo, Meddie Kagere amepewa kazi maalumu na Patrick Aussems ya kufanya dhidi ya Azam FC.

Aussems amemkabidhi Kagere jukumu la kuhakikisha Azam anakufa mapema kadri inavyowezekana Jumatano ijayo.

 

Katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Aussems alifanya kikao na Kagere akimpatia mikakati ya kufanya kwa ajili ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka hapa nchini.

 

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusiana na hilo Aussems alisema kuwa: “Ni mambo ya kiufundi ambayo tulikuwa tukizungumzia sababu wiki ijayo tutakuwa na mchezo mgumu dhidi ya Azam.

 

“Kwa hiyo ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huo tunatakiwa kujipanga ndiyo maana tunajiandaa kwa kila jambo,” alisema Aussems. Kwa sasa Kagere katika kikosi cha Simba, ndiye mshambuliaji tegemeo kwani ameifungia timu hiyo mabao sita.

Comments are closed.