Kagere: Kwa Simba Hii, Haponi Mtu

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere ameangalia mabadiliko ya kikosi hicho kutokana na usajili uliofanywa kisha akatoa kauli kuwa safari hii hakuna atayeweza kupona katika mechi zao.

 

 

Kagere ambaye ni mfungaji bora wa msimu uliopita baada ya kufanikiwa kufunga mabao 23 katika Ligi Kuu Bara huku akifunga mabao sita katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mshambuliaji huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuanza maandalizi ya kambi ya pamoja inayoendelea nchini Afrika Kusini kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kagere alisema; “Tumeanza maandalizi vizuri kila mchezaji amekuwa akijituma katika mazoezi kwa ajili ya kutafuta namba katika kikosi cha kwanza, ushindani umekuwa mkubwa naamini kwetu ni jambo zuri ambalo litasaidia kuendelea kuwa bora zaidi ya msimu uliopita.”

 

“Hakuna atakayeweza kutoka kwetu kwa sababu tunaangalia kutetea ubingwa na kufika mbali katika michuano ya kimataifa, matumaini yangu ni kuendelea kufanya vizuri katika kila mechi kwa sababu nataka kufikia rekodi yangu ya msimu uliopita kwa kufunga mabao,” alisema Kagere ambaye ana asili ya Uganda.


Loading...

Toa comment