Kagere: Makambo ametangulia tu

Meddie Kagere

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere amemchimba mkwara mpinzani wake katika mbio za kuwania ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara, Harietier Makakambo wa Yanga kwa kusema kuwa hata afunge mabao mangapi lakini hawezi kutwaa tuzo hiyo zaidi yake.

 

Kagere mwenye mabao 14 akizidiwa bao moja na Makambo mwenye mabao 15 wakati anayeongoza ni mshambuliaji wa Mwadui, Salim Aiyee akiwa amefunga mabao 16 licha ya timu yake kuwa katika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kutokana na kuwa na pointi 37.


Akizungumza na Spoti Xtra, Kagere alisema kuwa hawezi kuwa na presha na suala la ufungaji katika ligi kuu kutoka kwa wapinzani wake akiwemo Makambo kutokana na kuamini nafasi kubwa ipo kwake.

 

“Siwezi kuwa na presha ya nani amefunga mabao mangapi kwa sababu hii ni ligi na kila mmoja anacheza kwa kuipambania timu yake hivyo kwangu naona ni jimbo la kawaida kwa kuwa bado nina nafasi kubwa ya kuweza kufunga mabao zaidi ya wao kulingana na mechi zilizopo mbele yetu.

 

 

“Najua nini cha kufanya ili kuweza kutimiza hilo, mabao nitafunga na nitakua juu ya hao ambao wamenizidi, yeye namuacha aendelee kufunga na nitafunga yangu kutokana na ushirikiano ninaoupata kutoka kwa wachezaji wenzangu hilo halitokuwa na shida ni suala muda kufika tu,” alisema Kagere.

Loading...

Toa comment