The House of Favourite Newspapers

Kagere Ndani, Morrison Freshi, Sasa Kazi Kwisha!

0

HABARI mbaya kwa wapinzani wa Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Plateau United ya Nigeria ni kuwa, straika mwenye njaa ya mabao, Meddie Kagere amejumuishwa kwenye msafara utakaoenda kupambana na kikosi hicho nchini Nigeria.

 

 

Straika huyo amejumuishwa kwenye kikosi hicho na anatarajiwa kuanza kazi yake ya kutupia mabao baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu na kukosa mechi kadhaa za Ligi Kuu Bara ikiwemo dhidi ya Yanga.

 

 

Kagere alikuwa nje ya dimba baada ya kuumia dhidi ya JKT Tanzania ambapo aliwakosa Prisons, Ruvu Shooting, Kagera Sugar, Mwadui, Yanga na Coastal Union. Kati ya Novemba 27-29, mwaka huu, Simba watacheza na Plateau United mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini nchini Nigeria, kisha marudiano ni kati ya Desemba 4-6, mwaka huu jijini Dar. Mechi hizo ni za hatua ya awali.

 

 

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck, amesema: “Kila mchezaji atakuwepo kwenye mechi ya Nigeria akiwemo Kagere ambaye hakuwepo kwenye mechi zilizopita, hakuna ambaye tutamkosa zaidi ya wale wenye majeraha ya muda mrefu.”

 

 

Wakati huohuo, uongozi wa Klabu ya Simba umeibuka na kusema kuwa tayari umeshatuma jina la Mghana, Bernard Morrison katika usajili wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya michuano hiyo.

 

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Simba, Abbas Ally, amesema: “Dirisha la usajili wa Caf lilifunguliwa Oktoba 30, mwaka huu na kuchukua siku chache kabla ya kufungwa. Kwa upande wetu tumewasilisha majina yote ya wachezaji tuliowasajili msimu huu akiwemo Morrison.

 

 

“Tunahitaji kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya kimataifa, kikosi chetu kipo vizuri lengo ni kuona tunafi kia malengo.”

Ikumbukwe kuwa, Yanga hivi karibuni iliibua tena sakata la mkataba wao na Morrison na kudai kwamba jina la mchezaji huyo halipo kwenye usajili wa mfumo wa TMS, Simba wanasubiri dirisha dogo lifunguliwe waliingize, hivyo wameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuliangalia suala hilo.

SAID ALLY NA KHADIJA, MNGWAI, Dar es Salaam

Leave A Reply