The House of Favourite Newspapers

KAHABA KUTOKA CHINA-05

0

Peter akaliegesha gari lake nje ya geti la kuingilia katika kambi ya kijeshi ya Lugalo. Kwa kuwa alikuwa ni mtoto wa mwanajeshi, akatoa kitambulisho chake na kisha kumuonyeshea mwanajeshi ambaye alimtaka kufanya hivyo na kisha kuruhusiwa. Akaliendesha gari lake mpaka katika sehemu ya maegesho na kisha kuteremka.

Kichwa chake kilikuwa kwenye mawazo mengi, hakuamini kwamba Bwana Shedrack hakuwa amemwambia Rose kile ambacho alikuwa ameambiwa na baba yake, Bwana Edward. Kitu ambacho alikijua ni kwamba kila kitu kingekuwa chepesi kwake, yaani kamakumsukuma mlevi katika mteremko wa mlima kumbe hali ilikuwa tofauti kabisa.

“Nipo hapa sehemu ya kuegeshea magari,” Peter alimwambia Bwana Shedrack.

“Sawa. Nakuja,” Bwana Shedrack alimwambia Peter simuni.

Peter akabaki akiwa amesimama ndani ya eneo lile huku akiwa ameegemea gari lake. Baada ya dakika tano, Bwana Shedrack akatokea mahali hapo na kisha kumsalimia.

“Naona mambo hayaendi vizuri mzee” Peter alimwambia Bwana Shedrack baada ya kuongea maongezi machache.

“Kivipi?”

“Kuhusu Rose.”

“Amefanya nini tena?”

“Nimetoka kwako hapa na nimeongea naye,” Peter alimwambia bwana Shedrack.

“Kasemaje?” Bwana Shedrack aliuliza huku akionekana kuwa na furaha.

“Kanikataa.”

“Kakukataa! Kivipi?”

“Sijui. Yaani inaonekana kwamba haujamwambia kitu chochote kile,” Peter alisema kinyonge.

“Hapana. Nilimwambia. Tena nilimwambia kila kitu,” Bwana Shedrack alimwambia Peter.

“Basi ndio hivyo. Kanikataa,” Peter alimwambia Bwana Shedrack.

Bwana Shedrack akaonekana kuchanganyikiwa, hakuamini kile ambacho Peter alikuwa amekisema ndicho ambacho kilikuwa kimetokea. Moyoni mwake alikuwa na uhakika kwamba kwa jinsi alivyokuwa ameongea na binti yake, Rose mpaka kwa wakati huo kila kitu kingekuwa safi yaani ingebakia kitendo cha Peter kuja na kuongea maneno machache ya kumalizia.

Bwana Shedrack hakutaka kuendelea kuongea na Peter, alichokifanya ni kuondoka mahali hapo, akaingia ndani ya gari na kuelekea nyumbani kwake. Ndani ya gari, hasira zake zilikuwa juu ya Rose tu. Ni kweli alijua kwamba hakutakiwa kumlazimisha binti yake katika kupanga maamuzi ya maisha yake lakini katika suala kama hilo, suala la kuufanya ukaribu wake na Bwana Edward kuzidi kushamili, aliona ana kila sababu ya kumlazimisha Rose kukubaliana nae hata kama alikuwa akifanya makosa.

“Hawa watoto wengine bwana, wanataka kuniaibisha mtu mzima,” Bwana Shedrack alijisemea huku akionekana kuwa na hasira.

Njia nzima Bwana Shedrack alionekana kuwa na mawazo mengi, kichwa chake kilikuwa kikimuuma sana kwa ajili ya kumfikiria binti yake ambaye alikuwa amemkataa Peter. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kukifanya kwa wakati huo, hakujua ni hatua gani madhubuti ambazo alitakiwa kuzichukua mara atakapofika nyumbani.

Alipofika nyumbani, akaliegesha gari na kisha kuingia ndani. Siku hiyo Bwana Shedrack alionekana kubadilika sana, alionekana kuwa mwingi wa hasira kupita kawaida. Alipofika ndani, macho yake yakatua kwa John ambaye alikuwa akiangalia televisheni sebuleni.

“Shikamoo baba,” Joh alimsalimia.

“Dada yako yupo wapi?” Bwana Shedrack aliuliza huku akionekana kuwa na hasira.

“Yupo chumbani kwake,” John alijibu huku akionekana kuwa na wasiwasi.

Bwana Shedrack hakutaka kuongea kitu kingine chochote kile, alichokifanya ni kuanza kuelekea ukumbini na alipoufikia mlango wa chumba cha Rose akaanza kuugonga. Alisimama na kuugonga kwa muda mrefu lakini haukufunguliwa wala kusikia sauti ya mtu yeyote ndani jambo ambalo lilimfanya kuingia ndani, alipoingia, hakukuwa na mtu yeyote yule.

Bwana Shedrack hakuishia hapo, akaanza kwenda katika kila sehemu, akaelekea jikoni, akaelekea mpaka stoo, bafuni na chooni huko kota Rose hakuonekana. Hapo ndipo ambapo akaonekana kuwa na wasiwasi, akaelekea nje ya nyumba hiyo upande wa nyuma, alipoangalia geti, lilikuwa halijafungwa vizuri kitu ambacho alijua fika kwamba Rose alikuwa ametoka nje kupitia geti la nyuma, na kama alikuwa ametumia geti hilo ina maanisha kwamba hakutaka kuonekana na John. Alichokifanya akaanza kulifuata geti lile, alipotaka kulifunga tu, Rose akalifungua kutokea nje na kukutana uso kwa uso.

****

Mawazo ya Irene yalikuwa yakimfikiria Rose ambaye alikuwa amemuacha nyumbani, tayari aliona dhahiri kwamba uhusiano wake wa kimapenzi pamoja na Rose ulikuwa ukienda kuharibika muda si mrefu. Maneno ya Rose kwamba alikuwa akijisikia raha zaidi kila alipotumia kiungo wa bandia ndio ilikuwa kauli ambayo ilimtia sana wasiwasi.

Alijua fika kwamba kama asingefanya kazi ya zaidi basi alikuwa akienda kumpoteza Rose ambaye kwake alionekana kuwa msichana muhimu kwa sababu tu alimkuta bikira na hivyo hakutaka kumuachia. Kiungo wake wa bandia ambao alikuwa amemuachia alijua fika kwamba ule ndiio ambao ungeleta kizaazaa hapo baadae.

Kuna wakati mwingine alitamani sana kurudi nyumbani na kuuchukua kiungo ule lakini kila alipotaka kufanya hivyo,. Akapuuzia kwa kuona kwamba hakukuwa na umuhimu wowote ule. Hakujua, hakujua kwamba kile kitu ambacho alikuwa akikifikiria ndicho ambacho kilikuwa kikiendelea kufanya kazi akilini mwa Rose. Katika kipindi hicho, alikuwa na kiu ya kufanya mapenzi na mwanaume yeyote yule.

Siku ziliendelea kukatika mpaka siku ambayo alipokea simu na kupewa taarifa kwamba Rose alikuwa njiani kufunga ndoa na kijana Peter. Kwanza akashtuka, taarifa zile zilionekana kumshtua kupita kawaida. Ilikuwaje Rose aamue moja kwa moja kwamba anafunga ndoa pasipo kumtaarifu, Irene akaonekana kuchanganyikiwa sana.

Moyoni akashikwa na kimuemue cha kutaka kufahamu sababu ambayo ilimfanya Rose kukubali kufunga ndoa kirahisi bila kumfahamisha, akagundua kwamba kulikuwa na uwezekano wa Bwana Shedrack kumlazimisha kufunga ndoa ile. Irene haukutaka kuvumilia kubaki chuoni, alijiona kuwa na uhitaji wa kuonana na msichana huyo ambaye kila siku alikuwa akimuita mke wake na kuzungumza nae.

Ila kabla hajaamua kuelekea nyumbani huko, akachukua simu yake na kisha kuanza kumpigia Rose. Kwanza alitaka kufahamu kila kitu, sababu ambayo Rose aliamua kutaka kufunga ndoa na Peter na wakati alijua fika kwamba yeye alikuwepo kwa ajili yake. Simu ikaanza kuita, iliita kwa muda fulani na kisha kukatika. Irene hakutaka kuacha, akapiga tena, simu ikaanza kuita tena na hatimae kupokelewa.

“Ndio umefanya nini sasa?” Irene aliuliza bila hata kujua ni mtu gani alikuwa akiongea.

“Nakuuliza wewe. Ndio umefanya nini tena mpenzi. Yaani mahaba yote ambayo nilikupa kitandani, yaani kukichezea kifua chako chote, eti leo hii unakubali kuolewa na mwanaume, au haujui kwamba mimi ndiye mwanaume wako? Au haujui kwamba mimi ndiye mtu ambaye nimekutoa bikira kwa kutumia kiungo wa bandia? Hivi kwa nini unaamua kunisaliti Rose? Hivi kwa nini umeamua kufanya jambo kama hili kwangu. Au mjomba kakulazimisha? Na kama alikulazimisha kwa nini usiongeondoka nyumbani ukaja japo huku hosteli ukaja tukakaa pamoja? Umenikasirisha mke wangu, mahaba yangu yameonekana kuwa si kitu,” Irene aliongea kwa sauti ya hasira bila kusikia sauti ya upande wa pili.

“Umenikasirisha…umenikasirisha sana…umenisikia..halllow,” Irene alisema kwa hasira na kuita baada ya kutokuisikia sauti ya Rose.

“Endelea nakusikiliza,” sauti ya mwanaume ilisikika simuni, alikuwa Bwana Shedrack.

Irene akashtuka, hakuamini kwamba maneno yote ambayo alikuwa akiyaongea kumbe yalikuwa yakisikika masikioni mwa Bwana Shedrack ambaye alikuwa ameipokea simu ile. Kwa haraka sana bila kupoteza muda, akakata simu na kuizima kabisa.

Mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, hofu ikamuingia moyoni kwa kuona kwamba Bwana Shedrack alikuwa amefahamu kila kitu ambacho kilikuwa kimeendelea. Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, kila kitu kilikuwa wazi kwa Bwana Shedrack kitu ambacho kilimfanya kujilaumu sana kwa kuongea mfululizo bila kusikiliza sauti ya upande wa pili.

“Mmmh! Nitafanya nini sasa! Mjomba anaweza hata kuniua,” Irene alijisemea huku akionekana kuwa na hofu kubwa.

Kwa wakati huo, kila kitu kikaonekana kuwa wazi, Bwana Shedrack akaonekana kufahamu kila kitu ambacho kilikuwa kikitokea chumbani katika kipindi ambacho Irene alikuwa akielekea katika nyumba ile. Irene hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, kitendo cha mjomba wake kufahamu kila kitu kikaonekana kumtia hofu kupita kawaida.

 

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Alhamisi hapahapa.

Leave A Reply