Kaimu Mkurugenzi mpya Muhimbili akutana na kamati tendaji yake
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma (MNH), Aminiel Aligaesha (kulia) na akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali hiyo Profesa Lawrence Mseru kwa kamati tendaji, wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo ya Kibasila, Sewahaji, Mwaisela na Jengo la Watoto.
Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru (kulia) akizungumza na kamati tendaji, wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo ya Kibasila, Sewahaji, Mwaisela na Jengo la Watoto.
Kamati Tendaji, wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo ya Kibasila, Sewahaji, Mwaisela na Jengo la Watoto wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru.
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Hussein Kidanto (kushoto) akishukuru watumishi wa hospitali hiyo na kumtambulisha Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Mseru (kulia) ambaye ameteuliwa jana na Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru leo ameanza kazi na kuwataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwahi kazini kwa wakati na kufanya kazi kwa bidii.
Profesa Mseru ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam baada ya kukutana na menejimenti ya hospitali hiyo ambayo inajumuisha Wakurugenzi 14.
Mkurugenzi huyo amekutana na menejimenti hiyo majira ya saa 6:00 mchana katika ukumbi wa mikutano wa hospitali hiyo.
Pia, amekutana na kamati tendaji ya hospitali , wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo ikihusisha Sewahaji, Mwaisela, jengo la watoto na jengo la wazazi saa 8: 00 mchana.
Pamoja na mambo mengine katika kikao hicho, wakurugenzi wameeleza mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo.
Profesa Mseru ameteuliwa jana kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo baada ya Dk Hussein Kidanto kuhamishiwa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.