Kairuki Yaja na Teknolojia Kutibu Saratani Bila Upasuaji
Dk Fredy Rutachunzibwa wa Kairuki hospitali ambaye ni Mtanzania wa kwanza kufuzu mafunzo ya kutibu saratani kwa kutumia teknolojia ya HIFU (High-Intensity Focused Ultrasound), ameeleza namna tiba hiyo inavyotolewa bila upasuaji.
HIFU ni teknolojia ya kisasa inayotumia mawimbi ya sauti yenye nguvu kuteketeza seli za saratani kwa usahihi, bila kuhitaji upasuaji.
Akizungumza na gazeti hili jana, daktari huyo alisema mbinu hiyo inapunguza maumivu, hatari ya maambukizi na muda wa kupona kwa wagonjwa.
Alisema Hospitali ya Kairuki ni ya kwanza nchini Tanzania, Afrika Mashariki na Kati kutumia teknolojia ya HIFU, na ni ya tatu Barani Afrika.