The House of Favourite Newspapers

Kaizer Yaingilia Usajili Wa Straika Msauzi Yanga

0

IMEFAHAMIKA kuwa Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inahusishwa kuingia katika vita dhidi ya Yanga ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Marumo Gallants ya nchini humo, Ranga Chivaviro.

Chivaviro ni kati ya wachezaji wanaotajwa kuwepo katika rada za kusajiliwa na Yanga katika msimu ujao ambao wamepanga kufanya vizuri zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga inaihitaji saini ya mshambuliaji huyo anayetajwa kuchukua nafasi ya Mkongomani, Fiston Mayele ambaye inaelezwa huenda akauzwa nje ya nchi baada ya kupata ofa kadhaa.

Timu hiyo, ambayo msimu huu inacheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika huku wakiwa na uhakika wa kutinga fainali, baada ya kupata ushindi wa nyumbani mabao 2-0 kabla ya kurudiana na Marumo Gallants huko Afrika Kusini.

Taarifa kutoka Afrika Kusini zimethibitisha kuwa Kaizer imepanga kuwasajili wachezaji wapya tisa katika kukiimarisha kikosi hicho.

Wachezaji hao wanaowaniwa na Kaizer ni Mayele ambaye kama mazungumzo yakienda vizuri, basi atajiunga na timu hiyo.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said hivi karibuni alizungumzia usajili kwa kusema kuwa: “Tupo tayari kumsajili mchezaji yeyote kwa gharama yoyote kwa yule atakayehitajika na benchi la ufundi.

“Pia hatutakuwa tayari kumuachia mchezaji yeyote aliye katika mipango ya benchi la ufundi, kwani tupo katika mipango ya kuitengeneza timu itakayokuwa tishio na hatari Afrika,” alisema Hersi.

STORI NA WILBERT MOLANDI

Leave A Reply