KAJALA AANIKA MAUMIVU MWANAYE KUFELI

Kajala Masanja

STAA mkali wa filamu za Bongo Muvi, Kajala Masanja amefungukia baadhi ya kejeli na dharau anazorushiwa mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutofanya vizuri mtihani wake wa kumaliza kidato cha nne na kusema kuwa kama mama hapendezwi hata kidogo na kejeli hizo.  Akizungumza na Za Motomoto, Kajala alisema kuwa inasikitisha kuona watu wazima wanamrushia maneno makali mtoto wake na ya kumkatisha tamaa lakini yeye kama mzazi hawezi kumuacha asimuendeleze kwa sababu tu kafeli mtihani ambao anaamini hata wanaomtolea maneno mwanaye walifeli pia.

“Mimi kama mzazi siwezi kufurahi maneno wanaomrushia mwanangu kwa sababu hata kufeli kwake siyo sababu ya kushindwa kumuendeleza kielimu na mimi kama mama nitamsimamia Paula, mpaka atafika chuo kikuu na watu hawataweza kuamini na kingine wamuache mtoto wangu jamani,” alisema.

Stori: Imelda Mtema

Toa comment