Kajala Afunguka Kurogwa na Mpenzi Wake

MWIGAZAJI Kajala Masanja alikuwa gumzo mno alipokuwa kwenye makopa na Harmonize au Konde Boy Mjeshi, lakini baada ya kumwagana dizaini kama alipoa.

 

Hata hivyo, kwa sasa Kajala amethibitisha kuwa kwenye penzi jipya baada ya kusema; “Sijawahi kupenda kiasi hiki, this is too much, nina wasiwasi safari hii nitakuwa nimerogwa, aki nimerogwa…”

 

Kauli ya Kajala inathibitisha tetesi za wiki kadhaa kwamba hivi sasa ana mpenzi mpya ambaye ameamua kufanya siri asijulikane kama wanavyofanya waigizaji wenzake wa Bongo Movies, Irene Uwoya, Wema Sepetu, Shamsa Ford na wengine kibao.


Toa comment